AI: Kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Ethiopia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i61295-ai_kuna_ukiukwaji_mkubwa_wa_haki_za_binadamu_ethiopia
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema vikosi vya usalama nchini Ethiopia vinakiuka haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kujihusisha na mauaji ya kiholela na utesaji watu tangu Waziri Mkuu Abiy Ahmed achukue hatamu za uongozi mwaka 2018.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 29, 2020 23:25 UTC
  • AI: Kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Ethiopia

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema vikosi vya usalama nchini Ethiopia vinakiuka haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kujihusisha na mauaji ya kiholela na utesaji watu tangu Waziri Mkuu Abiy Ahmed achukue hatamu za uongozi mwaka 2018.

Katika taarifa iliyochapishwa Ijumaa, Amnesty International imesema imeorodhesha taarifa za kuwekwa kizuizini maelfu ya watu bila kufunguliwa mashtaka huku idadi kubwa ya familia zikitimuliwa kutoka katika makazi yao katika oparesheni za kukabiliana na wangamabo na mapigano ya kikabila katika maeneo ya Amhara na Oromia.

Ripoti hiyo inahusu ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka Disemba 2018 hadi Disemba 2019.

Wakimbizi wa ndani ya nchi nchini Ethiopia

Abiy Ahmed alianzisha marekebisho makubwa, ikiwa ni pamoja na kuwasamehe maelefu ya wafungwa wa kisiasa alipoingia madarakani Aprili 2018. Aidha alianzisha mchakato wa kuhitimisha uhasama na nchi jirani ya Eritrea na alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka jana kutokana na jitihada zake hizo.

Lakini kipindi cha uongozi wake kimegubikwa na mapigano ya kikabila ambayo yamepelekea malaki ya watu kuwa wa kimbizi wa ndani ya nchi huku hali ya usalama ikizidi kuwa mbaya.