Vikosi vya Usalama vimeua watu 200 eneo la Sahel barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i61519-vikosi_vya_usalama_vimeua_watu_200_eneo_la_sahel_barani_afrika
Vikosi vya ulinzi na usalama katika ukanda wa Sahel barani Afrika vimeua raia 200 kati ya mwezi Februari na Aprili mwaka huu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2020 07:34 UTC
  • Vikosi vya Usalama vimeua watu 200 eneo la Sahel barani Afrika

Vikosi vya ulinzi na usalama katika ukanda wa Sahel barani Afrika vimeua raia 200 kati ya mwezi Februari na Aprili mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Jumatano ya shirika la kimataifa ya haki za binadamu Amnesty International,  watu wasiopungua 199 waliuawa na vikosi vya ulinzi na usalama kati ya mwezi Februari na Aprili mwaka huu.

Ousmane Diallo, mtafiti wa shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Amnesty International amesema takwimu hizi ni makisio ya chini.

Diallo ameongeza kuwa inasemekana kuwa wanajeshi wa Mali, Niger na Burkina hawaheshimu haki za binadamu na sheria za kimataifa kuhusu suala hilo.

Ukanda wa Sahel

Ripoti ya Aprili ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali, MiNUSMA, pia inavishtumu vikosi vya Mali na Niger kwa kuwakandamiza raia.

Siku ya Ijumaa, shirika la haki za binadamu la Tabital Pulaaku, lilishtumu jeshi la Mali, kulingana na ushuhuda kuhusika kuteketezwa moto kijiji kimoja kinachopatikana katikati mwa nchi hiyo.

Nchi 5 za eneo la Sahel Afrika linalojumuisha nchi za Burkina Faso, Mali, Mauritania, Niger na Chad zinatekeleza operesheni kubwa dhidi ya makundi ya kigaidi katika ukanda huo.