Nchi kadhaa zatuhumiwa kutuma silaha Congo DR, nyingine zinatumwa kwa waasi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i61691-nchi_kadhaa_zatuhumiwa_kutuma_silaha_congo_dr_nyingine_zinatumwa_kwa_waasi
Umoja wa Mataifa umezituhumu baadhi ya nchi kwamba zinatuma silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bila ya kuutaarifu umoja huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 19, 2020 02:00 UTC
  • Nchi kadhaa zatuhumiwa kutuma silaha Congo DR, nyingine zinatumwa kwa waasi

Umoja wa Mataifa umezituhumu baadhi ya nchi kwamba zinatuma silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bila ya kuutaarifu umoja huo.

Ripoti mpya iliyowasilishwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imesema kuwa, jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linaendelea kupokea silaha na mafunzo ya kijeshi kutoka nje ya nchi kinyume na azimio la mwaka 2004 la baraza hilo.

Ripoti ya siri ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa ambayo imetolewa leo inaonyesha kuwa baadhi ya silaha hizo zinatumwa kwa makundi ya waasi huko mashariki mwa Congo DR. 

Eneo hilo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linasumbuliwa na mapigano na uasi wa miaka mingi ambao umesababisha mauaji ya maelfu ya watu na kuwalazimisha wengine zaidi ya nusu milioni kuwa wakimbizi katika miezi ya hivi karibuni. 

Miaka ya nyuma serikali ya Kinshasa ilikuwa ikizituhumu baadhi ya nchi jirani kuwa zinachochea machafuko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Nchi hizo kwa upande wao zinaituhumu Congo DR kuwa imekuwa maficho salama kwa magenge ya waasi