Afrika Kusini yakosoa madai ya viongozi wa Marekani dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i63427-afrika_kusini_yakosoa_madai_ya_viongozi_wa_marekani_dhidi_ya_iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini ameyataja madai yaliyotolewa na viongozi wa Marekani dhidi ya Iran kuwa hayana msingi wowote.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 14, 2020 22:07 UTC
  • Afrika Kusini yakosoa madai ya viongozi wa Marekani dhidi ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini ameyataja madai yaliyotolewa na viongozi wa Marekani dhidi ya Iran kuwa hayana msingi wowote.

Tovuti ya POLITICO imenukuu ripoti za kiintelijensia za Marekani na maafisa walio karibu na serikali ya nchi hiyo na kudai kuwa Iran inapanga kumuuwa Lana Marks, Balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini, Lunga Ngqengelele jana Jumatatu alifanya mahojiano na tovuti ya habari ya Blomberg ambapo alikosoa madai hayo yasiyo na msingi ya Marekani na kueleza kuwa: Dr Naledi Pandor Waziri wa Ushirikiano na Uhusiano wa Kimataifa wa nchi hiyo atatoa taarifa akieleza uongo wa  madai hayo.  

Dr Naledi Pandor, Waziri wa Ushirikiano na Uhusiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini  

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Sayyid Khatibzadeh pia jana alipinga tuhuma hizo za kichochezi na zinazotolewa kwa malengo maalumu dhidi ya Iran zilizochapishwa na katika vyombo vya habari vya Marekani.

Khatibzadeh amesema kuwa, viongozi wa Marekani wanapaswa kuache kutumia mbinu chafu za kukaririwa kwa shabaha ya kueneza proganda chafu dhidi ya Iran kimataifa. Ameongeza kuwa, Iran ikiwa ni nchi mwanachama inayowajibika  katika jamii ya kimataifa, imethibitisha kuheshimu kwake sheria na kanuni za kidiplomasia za kimataifa.