Rwanda kuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i6433-rwanda_kuwa_mwenyeji_wa_mkutano_wa_viongozi_wa_umoja_wa_afrika
Rwanda iko tayaria kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika AU baadaye mwaka huu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 05, 2016 03:55 UTC
  • Rwanda kuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika

Rwanda iko tayaria kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika AU baadaye mwaka huu.

Hayo yamebainika baada ya kutiwa saini mapatano baina ya Balozi wa Rwanda nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika Hope Tumukunde na Djeneba Diarra Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika.

Tumukunde amesema kutiwa saini mapatano hayo ni urasimu tu kwani Rwanda inafanya kila linalotakiwa ili kufanyika mkutano wa AU mjini Kigali unafana.

Kwa upande wake, Djeneba Diarra amesema hana shaka kuwa Rwanda iko tayari kwa ajili ya mkutano huo. Amesema alitembelea Kigali Machi mwaka jana kutathmini utayarifu wa Rwanda kuandaa mkutano huo wa kihistoria na kwamba mji huo uko katika kasi ya kuweka suhula zote tayari kwa ajili ya kikao hicho.

Mkutano wa Kilele wa AU unatazamiwa kuwaleta pamoja watu 3,500 mjini Kigali wakiwemo viongozi wa nchi wanachama, Tume ya Umoja wa Afrika pamoja na wawakilishi wa mashirika kadhaa ya AU.