Harakati ya Polisario yashambulia ngome za jeshi la Morocco
(last modified Sat, 28 Nov 2020 04:40:46 GMT )
Nov 28, 2020 04:40 UTC
  • Harakati ya Polisario yashambulia ngome za jeshi la Morocco

Harakati ya Polisario imezishambulia ngome za Morocco katika eneo la Karkarat kusini mwa Sahaha Magharibi.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mapigano yanaendelea kati ya Harakati ya Polisario na jeshi la Morocco zikiwa zimepita wiki mbli tangu kufunguliwa kivuko cha mpakani cha Karkarat kusini mwa Sahara Magharibi. 

Eeneo la Sahara magharibi huko kusini mwa Morocco 

Jeshi la Morocco limejenga matuta katika eneo la Karkarat kusini mwa Sahara kwa lengo la kurahisisha usafiri wa malori ya bidhaa yanayotumia kivuko cha mpakani cha Karkarat. Safari za malori baina ya Morocco na Mauritania zimeanza tena pamoja na kujengwa matuta hayo yaliyotajwa na Harakati ya Polisario kuwa ya fedheha. 

Harakati ya Polisario imeitaja hatua hiyo ya Morocco kuwa ya kichokozi na ndio maana harakati hiyo imetekeleza mashambulizi katika ngome za jeshi la nchi hiyo. 

Harakati hiyo imetoa taarifa na kueleza kuwa wapiganaji wake wamezishambulia ngome za jeshi la Morocco kwa silaha nzito na kuvisababishia hasara vikosi vamizi. Harakati ya Polisario ni taasisi ya kisiasa na kijeshi  inayoundwa na watu kutoka Sahara Magharibi huko kaskazini magharibi mwa Afrika na kusini mwa Morocco ambayo inaendesha mapambano kwa ajili ya uhuru wa eneo hilo. 

Tags