Wapinzani Sudan wataka kufanyika maandamano dhidi ya serikali
(last modified Mon, 14 Dec 2020 07:47:51 GMT )
Dec 14, 2020 07:47 UTC
  • Wapinzani Sudan wataka kufanyika maandamano dhidi ya serikali

Sambamba na ziara ya Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Sudan nchini Ethiopia, wapinzani nchini Sudan wamewatolea wito wananchi kufanya maadnamano tarehe 19 mwezi huu.

Chama cha Kikomonisti cha Sudan na baadhi ya kamati za muqawama za nchi hiyo zimetaka kufanyika maandamano hayo tajwa kwa lengo la kuifuta katiba na kuengua idara mbili za kiraia na kijeshi ndani ya serikali ya mpito ya nchi hiyo. Wapinzani nchini Sudan sambamba na kuadhimisha maandamano ya mamilioni ya wananchi nchini humo yaliyofanyika mwaka juzi wa 2018 wametaka kufanyiwa marekebisho mchakato wa mapinduzi na kutimizwa malengo ya mapinduzi hayo ya Wasudan.  

Jaadar Hassan mmoja wa viongozi wa Harakati ya Uhuru na Mabadiliko na Msemaji wa Jumuiya ya Shirikisho la Sudan  amesema  anataraji kuwa, maadhimisho ya mwaka wa pili wa mapinduzi ya wananchi ya mwezi Disemba yawe ni siku ya kutathmini mafanikio ya serikali ya mpito ya Sudan. 

Abdallah Hamdok Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Sudan jana Jumapili alielekea Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia akiwa katika ziara rasmi nchini humo. Maandamano ya wananchi wa Sudan ya kulalamikia hali mbaya ya kiuchumi chini ya uongozi wa Omar al Bashir yalianza mwezi Disemba mwaka 2018. Aidha Rais Omar al Bashir alipinduliwa madarakani mwaka jana 2019 kufuatia uingiliaji wa jeshi baada ya kupamba moto maandano ya wananchi dhidi yake; na kisha likaundwa Baraza la Kijeshi la kuiongoza Sudan chini ya uongozi wa Abdulfattah al Burhan. 

Omar Hassan al Bashir, Rais wa Sudan aliyepinduliwa madarakani 

Licha ya kuwepo serikali ya mpito huko Sudan lakini hali ya mambo nchini humo bado si shwari, huku  ikiendelea kukabiliwa na mivutano hata baada ya kupinduliwa Rais Omar Hassan al Bashir. 

Tags