Wafanyakazi watatu wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakombolewa DRC
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i6589-wafanyakazi_watatu_wa_shirika_la_msalaba_mwekundu_wakombolewa_drc
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limesema kuwa, wafanyakazi watatu wa shirika hilo waliokuwa wametekwa nyara mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekombolewa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 07, 2016 11:38 UTC
  • Wafanyakazi watatu wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakombolewa DRC

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limesema kuwa, wafanyakazi watatu wa shirika hilo waliokuwa wametekwa nyara mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekombolewa.

Shirika la habari la Ufaransa AFP limemnukuu Alessandra Menegon, mkuu wa kazi za Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu nchini DRC akisema leo mjini Kinshasa kuwa amefurahishwa sana na kuona wafanyakazi hao wamerejea kwa familia zao. Vile vile amewashukuru viongozi wa serikali, wananchi na wakuu wa kikabila na kidini kwa msaada wao uliofanikisha kukombolewa wafanyakazi hao.

Kwa upande wake, Elisabeth Cloutier, msemaji wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu mjini Goma, makao makuu ya mkoa wa Kivu Kaskazini huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa, hakuna fedha zozote zilizotolewa kwa ajili ya kukombolewa wafanyakazi hao.

Wiki iliyopita, Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu lilitangaza habari ya kutekwa nyara wafanyakazi wake watatu na watu wenye silaha wasiojulikana katika eneo la Rutshuru katika mkoa wa Kivu Kaskazini.