Marekani inaendelea kuingilia Somalia kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i66400-marekani_inaendelea_kuingilia_somalia_kijeshi
Kamandi ya Oparesheni Maalumu za Jeshi la Marekani barani Afrika imetangaza kuwa, Jeshi la Marekani limeanza kutoa mafunzo tena kwa Jeshi la Somalia hata baada ya kutangaza kuondoa askari wake katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 02, 2021 22:58 UTC
  • Marekani inaendelea kuingilia Somalia kijeshi

Kamandi ya Oparesheni Maalumu za Jeshi la Marekani barani Afrika imetangaza kuwa, Jeshi la Marekani limeanza kutoa mafunzo tena kwa Jeshi la Somalia hata baada ya kutangaza kuondoa askari wake katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Kwa mujibu wa Meja Jenerali Dagvin Anderson, Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Somalia Afrika, siku ya Jumalili Jeshi la Marekani lilishiriki katika utoaji mafunzo kwa askari wa serikali ya Somalia.

Amedia kuwa, uamuzi wa kutoa mafunzo hayo ni ishara kuwa eti Jeshi la Marekani linafungamana na ahadi zake kwa Somalia na washirika wa eneo katika kukabiliana na wale wenye 'misimamo mikali'.

Wataalamu wa mambo wanasema kuwa, mapatano baina ya Marekani na Somalia yanaipa Washington idhini ya kutoa mafunzo, kushauri na kuunga mkono Jeshi la Somalia kwa njia mbali mbali. Aidha mapatano hayo yanalipa  Jeshi la Marekani haki ya kushiriki katika oparesheni za pamoja na askari wa Somalia.

Disemba mwaka jana, Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, ilitangaza kuwa, rais wa wakati huo Donald Trump alikuwa ametoa amri ya kuondolewa askari 700 wa Marekani nchini Somalia.

Pentagon iliongoeza kuwa aghalabu ya askari wa Marekani wangeondoka Somalia lakini kwamba askari wachache wangebakia Mogadishu kutoa ushauri kwa Jeshi la Somalia. Lakini hivi sasa haijaweza kubainika wazi idadi ya askari wa Marekani waliosalia Somalia na wale waliotumwa katika nchi jirani kama vile Kenya.

Kamandi ya Jeshi la Marekani Barani Afrika (AFRICOM) imetoa taarifa na kusema mwaka uliopita ilitekeleza mashambulizi zaidi ya 51 nchini Somalia.