Amir Abdolahian: Iran itaendelea kuiunga mkono Syria kwa nguvu zote
Msaidizi maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, Tehran itaendelea kuiunga mkono kwa nguvu zote serikali ya Syria.
Amir Abdolahian, Msaidizi maalum wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesema hayo katika mazungumzo yake na Shafiq Dayoub, balozi wa Syria hapa mjini Tehran na kueleza kwamba, Marekani kwa kutekeleza vikwazo vya kiuchumi imekuwa ikiendesha vita vya kigaidi dhidi ya Iran kwa kutumia ugaidi wa kiuchumi.
Msaidizi maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amebainisha pia katiika mazungumzo yake hayo na balozi Shafiq Dayoub kwamba, Syria na Iran zimekuwa na uhusiano mkongwe wa kirafikii na kidugu.
Kadhalika Amir Abdolahian, amesema kuwa, Syria ipo mstari wa mbele katika kambi ya muqawama na kwamba, Iran ipo pamoja na nchi hiyo na itaendelea kuiunga mkono kwa nguvu zake zote.
Msaidizi maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa ameashiria siasa haribifu za Marekani na uingiliaji wake katika masuala ya ndani ya nchi za eneo na kueleza kwamba, hii leo Marekani inazungumzia suala la kutaka mazungumzo ya moja kwa moja na Iran, lakini inachopaswa kufanya kwa sasa si kingine bali ni kuliondolea taifa hili vikwazo vyote na kkulitekeleza hilo kivitendo.