Wanachama wa Harakati ya Kiislamu Nigeria washiriki matembezi ya Siku ya Quds
(last modified Sat, 08 May 2021 12:21:59 GMT )
May 08, 2021 12:21 UTC
  • Wanachama wa Harakati ya Kiislamu Nigeria washiriki matembezi ya Siku ya Quds

Wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria jana Ijumaa walijitokeza kwa wingi katika matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika miji mikubwa ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Jimbo la Bauchi la kaskazini mashariki mwa nchi ndilo lililotia fora kwa kuwa na idadi kubwa ya waandamanaji katika matembezi ya mwaka huu.

Waandamanaji hao walisikika wakipiga nara za kuwaunga mkono na kuwateta wananchi madhulumu wa Palestina, huku wakilaani dhulma na uporaji wa ardhi za Wapalestina unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Soheila Zakzaky, binti ya Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky amesema harakati hiyo inaliona kuwa wajibu suala la kuwaunga mkono na kuwahami wananchi wasio na ulinzi wa Palestina.

Amesema hakuna kitu kitazuia Waislamu wa Kishia na wapenda haki nchini humo kufanya vikao na matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds iliyoadhimishwa jana Ijumaa katika pembe mbali mbali za dunia.

Mamilioni ya Wayemen katika maandamano ya Siku ya Quds

Harakati hii ya Kiislamu imekuwa ikifanya maandamano ya matembezi ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina katika siku hii kila mwaka.

Kadhalika wananchama wa harakati hiyo kwa mara nyingine wametumia jukwaa hilo kutoa mwito wa kuachiwa huru mara moja kiongozi wao, Sheikh Ibrahim Zakzaky.