May 22, 2021 06:35 UTC
  • Mkuu wa genge la Boko Haram ajipiga risasi kutaka kujiua Nigeria

Serikali na jeshi la Nigeria limethibitisha habari zinasosema kuwa, Abubakar Shekau, mkuu wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram amejipiga risasi begani katika jaribio la kutaka kujiua. Hii ni katika hali ambayo vyombo vingi vya habari vimeripoti kuwa, Shekau amejiua.

Gazeti la Wall Street Journal la  nchini Marekani limedai kuwa, Abubakar Shekau amejiua baada ya kuona amezingirwa kila upande na hakuna njia yoyote ya kukwepa kukamatwa akiwa hai.

Nalo shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, jeshi la Nigeria linafanyia uchunguzi habari zilizoenea kuwa Shekau amejiua. Baada ya hapo jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limepata habari za uhakika kwamba Shekau amejipiga risasi begani katika jitihada za kujiua, ingawa hata hivyo, hadi wakati tunaandaa habari hii, jeshi na serikali ya Nigeria ilikuwa bado haijathibitisha kifo cha kiongozi huyo wa Boko Haram ambaye habari za kifo chake zimekuwa zikitangazwa mara kwa mara na baadaye huzuka na kukanusha habari hizo.

boko

Genge la Boko Haram linafanya jinai kubwa dhidi ya wananchi wa Nigeria na nje ya Nigeria

 

Msemaji wa jeshi la Nigeria amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa, jeshi hilo linafanya uchunguzi wa kina kuhusu madai ya kujiua Abubakar Shekau.

Siku ya Jumatano, taasisi ya taarifa za kijasusi ya Nigera ilitangaza kuwa, Shekau amejipiga risasi na kujiua ili kukwepa asikamatwe.

Siku chache zilizopita pia, jeshi la Nigeria lilitangaza kuwa, limeua wanamgambo wasiopungua 9 wa Boko Haram baada ya wanamgambo hao kujaribu kufanya shambulio la uharibifu katika mji wa Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno.

Taarifa ya jeshi la Nigeria ilisomwa na Brigedia Jenerali Mohammed Yerima ambaye pia alisema kuwa, wanamgambo wa Boko Haram walikimbia kwenye eneo hilo baada ya kupata hasara kubwa na wengi wao kujeruhiwa kwa risasi.

Tags