May 15, 2016 06:45 UTC
  • Jeshi la DRC laanzisha operesheni mpya dhidi ya waasi wa Uganda

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeanzisha opereseheni mpya ya kijeshi dhidi ya waasi wa Uganda, mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua, jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kusaidiwa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, jana Jumamosi lilianzisha opereseheni ya pamoja ya kijeshi ya kupambana na waasi wa Uganda, mashariki mwa nchi hiyo.

Mac Azukayi, kamanda wa opereseheni ijulikanayo kwa jina la "Sokola 1" amesema kuwa, operesheni hiyo mpya ya jeshi la Kongo DR imeanza katika eneo la Eringeti, mjini Beni na lengo lake ni kuwamaliza kabisa waasi wa ADF wa Uganda wanaofanya mauaji mashariki mwa Kongo.

Operesheni hiyo imeanza baada ya waasi hao wa Uganda kuua karibu watu 50 katika mkoa wa Ituri wa kaskazini mashariki mwa Kongo na mkoa wa Kivu Kaskazini wa mashariki mwa nchi hiyo.

Jumuiya za kijamii za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimesema kuwa, maelfu ya watu wameuawa kwenye mji wa Beni katika mashambulizi ya mara kwa mara ya waasi, tangu mwaka jana hadi hivi sasa.

Tags