Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel kuitembelea Morocco
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i73222-waziri_wa_mambo_ya_nje_wa_israel_kuitembelea_morocco
Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel anatazamiwa kufanya safari ya kuitembelea Morocco wiki ijayo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 06, 2021 20:36 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel kuitembelea Morocco

Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel anatazamiwa kufanya safari ya kuitembelea Morocco wiki ijayo.

Vyanzo vya habari katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Morocco vimedokeza kuwa, Yair Lapid, Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni ataitembelea nchi hiyo ya Kiarabu ya kaskazini mwa Afrika baina ya Agosti 11-12.

Waziri huyo hivi karibuni alisema atafanya eti safari ya kihistoria nchini Morocco, siku chache baada ya Rabat kuruhusu ndege ya kwanza ya utawala wa Kizayuni kutua katika ardhi yake mwezi uliopita wa Julai.

Haya yanajiri huku maelfu ya watu wa Morocco wawakiendeleza kampeni katika mitandao ya kijamii ya kutaka David Govrin, mwakilishi wa Israel nchini Morocco atimuliwe mara moja.

Yair Lapid, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel

Disemba mwaka jana Morocco na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel zilisaini mapatano ya kuanzisha uhusiano baina yao na kisha Marekani ikatambua rasmi mamlaka ya udhibiti wa Morocco kwa eneo la Sahara Magharibi. 

Morocco ni nchi ya sita ya Kiarabu baada ya Jordan, Misri, Imarati, Bahrain na Sudan  kuanzisha uhusiano kati yake na utawala ghasibu wa Kizayuni.  Kitendo hicho cha Morocco cha kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel ambacho ni sawa na kusaliti malengo ya Palestina kimekabiliwa na radiamali hasi katika Ulimwengu wa Kiislamu na hata ndani ya Morocco kwenyewe.