Rais Kenyatta anawataka Wakenya kutekeleza jukumu lao katika kulinda usalama wa nchi
Rais Uhuru Kenyatta amekumbusha Wakenya kutekeleza jukumu lao la kiraia la kuilinda nchi akisema usalama wa Kenya, uhuru wake na ustawi sio suala makhsusi kwa taasisi za usalama za serikali.
“Jamii zetu na kwa hakikai, kila raia lazima atekeleza jukumu lake. Kwa hivyo, natoa wito kwa jamii na uongozi kushirikiana na vyombo vya usalama ili kutimzia malengo yetu”, amesema Rais Kenyatta.
Akizungumza leo Alhamisi katika Kituo cha Jeshi la Majini cha Mand Bay kwenye Kaunti ya Lamu, Rais wa Kenya amesema changamoto mbalimbali za kiusalama zinazoikabili nchi zinalazimu kuwepo ushirikiano mkubwa kati ya raia na vyombo vya usalama vya taifa.
Amesema, Kambi ya Jeshi la Wanamaji la Kenya ya Manda Bay ina umuhimu mkubwa katika kuimarisha juhudi za kupambana na ugaidi na kudhamini usalama wa baharini, pamoja na kulinda miundombinu ya bandari ya nchi hiyo.
Rais Kenyatta ameongeza kuwa kambi hiyo inaimarisha usalama katika eneo hilo na kulinda njia muhimu za kibiashara ambazo ni muhimu sana kwa biashara ya kimataifa.
Amesema kwa kuzingatia uwekezaji unaokua katika eneo hilo la pwani mwa Kenya, Manda ni mnara wa kusikiliza na kutazama wenye thamani kubwa kwa Kenya na Wakenya.