Mawakili wa Tunisia wataka kuanzisha uhusiano na Israel kutambuliwe kuwa ni uhalifu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i82922-mawakili_wa_tunisia_wataka_kuanzisha_uhusiano_na_israel_kutambuliwe_kuwa_ni_uhalifu
Kituo cha Taifa cha Mawakili nchini Tunisia kimewataka viongozi wa nchi hiyo kulitambua suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel kuwa ni jinai na uhalifu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 26, 2022 03:12 UTC
  • Mawakili wa Tunisia wataka kuanzisha uhusiano na Israel kutambuliwe kuwa ni uhalifu

Kituo cha Taifa cha Mawakili nchini Tunisia kimewataka viongozi wa nchi hiyo kulitambua suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel kuwa ni jinai na uhalifu.

Taarifa ya mawakili hao imeeleza kuwa, kuna haja ya kupasishwa sheria inayolitambua suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel kuwa ni uhalifu.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeitaka serikali ya Tunis kulaani hujuma, mashambulio na jinai za utawala vamizi wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Kituo hicho cha kisheria kisilicho cha kiserikali kimeeleza wasiwasi mkubwa kilionao wa kuendelea hujuma na mashambulio ya kila uchao ya jeshi la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesisitiza juu ya udharura wa kuchukuliwa hatua za kila upande kupinga vikali mwenendo wa baadhi ya mataifa ya Kiarabu wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo haramu

Maandamano ya kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel

 

Ikumbukwe kuwa, nchi nne za Kiarabu za Imarati (UAE), Bahrain, Morocco na Sudan mwaka 2020 zilisaini hati za makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni, hatua ambayo imeendelea kupingwa na kulaaniwa vikali katika nchi za Kiarabu na Kiislamu.

Sudan, Morocco na Bahrain zimeendelea kushuhudia maandamano kila leo ya wananchi ya kulaani na kupinga hatua ya nchi zao ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa  Israel. Wananchi waliowengi katika nchi hizo wanasema kuwa, hatua hiyo ni khiyana na usaliti mkubwa kwa wananchi wa Palestina wanaofanyiwa unyama wa kila aina na utawala wa Israel kila uchao.