Mgororo wa njaa wayakumba maeneo ya Ziwa Chad
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9193-mgororo_wa_njaa_wayakumba_maeneo_ya_ziwa_chad
Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu imetangaza kuwa watu zaidi ya milioni 9 wa eneo la Ziwa Chad barani Afrika wanahitaji misaada ya dharura ya kibinadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 14, 2016 09:49 UTC
  • Mgororo wa njaa wayakumba maeneo ya Ziwa Chad

Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu imetangaza kuwa watu zaidi ya milioni 9 wa eneo la Ziwa Chad barani Afrika wanahitaji misaada ya dharura ya kibinadamu.

Mkurugenzi wa Operesheni za Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, Dominica Stylhart amesema katika ripoti yake mpya kwamba watu milioni 9 wanahitaji misaada ya dharura ya kibinadamu katika eneo la Ziwa Chad kutokana na mapigano ya miaka 6 kati ya jeshi la serikali ya Chad na waasi wanaotumia silaha katika nchi za Niger, Chad, Cameroon na Nigeria.

Dominica Stylhart ameongeza kuwa, mgogoro wa njaa ni mkubwa sana hususan katika maeneo ambako misaada ya kibinadamu haijafika na kwamba kila siku watoto wanafariki dunia kutokana na utapiamlo.

Ripoti zinasema hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya kaskazini mwa Nigeria ambako mamia ya wakimbizi wanasumbulia na ukosefu wa chakula.