Waliouawa katika mashambulio ya kigaidi Somalia wapindukia 30
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i92518-waliouawa_katika_mashambulio_ya_kigaidi_somalia_wapindukia_30
Idadi ya wahanga wa milipuko miwili ya mabomu katika mji wa Mahas katikati ya Somalia imeongezeka na kufikia watu 30.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 05, 2023 03:36 UTC
  • Waliouawa katika mashambulio ya kigaidi Somalia wapindukia 30

Idadi ya wahanga wa milipuko miwili ya mabomu katika mji wa Mahas katikati ya Somalia imeongezeka na kufikia watu 30.

Hassan-Kafi Mohamed Ibrahim, Naibu Kamishna wa Polisi katika jimbo la Hirshabelle amesema, waliouawa katika mashambulio hayo ya kigaidi ya jana Jumatano ni 35, wakiwemo watu wanane wa familia moja.

Amesema watu wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa katika milipuko hiyo miwili ya mabomu ya kutegwa ndani ya gari iliyotokea kwa wakati mmoja mapema jana Jumatano katika mji wa Mahas kwenye mkoa wa Hiran katikati mwa Somalia. 

Watu walioshuhudia hujuma hiyo wameeleza kuwa milipuko hiyo ilitokea mkabala wa mgawaha mmoja karibu na ofisi ya mkuu wa wilaya katika mji wa Mahas ambapo wanawake na watoto ni kati ya wahanga tisa waliopoteza maisha. 

Hujuma hiyo ya jana katikati mwa Somalia inadaiwa kufanywa na kundi la kigaidi la al-Shabaab ambalo limekuwa likifanya mashambulizi dhidi ya serikali ya Mogadishu na kuwauwa watu tangu mwaka 2006. 

Magaidi wa al-Shabaab wanaowahangaisha raia na maafisa usalama wa Somalia na nchi jirani

Genge hilo la ukufurishaji limetangaza kuhusika na jinai hiyo n kudai kuwa, idadi ya watu waliouawa katika hujuma hiyo ya jana Jumatano ni 87, eti wakiwemo wanajeshi wasaliti wa Somalia na mamluki wao.

Mumin Mohamed Halane, Mkuu wa Wilaya ya Mahas amesema bomu moja lililenga makazi yake na jingine lililenga nyumba ya mmoja wa wabunge wa nchi hiyo ya Pemba ya Afrika na mashambulizi hayo ya jana ya al-Shabaab.