Mchambuzi wa Kiafrika apongeza kuimarika diplomasia ya Iran
Mchambuzi wa masuala ya kimataifa raia wa Nigeria amesema kuwa, Iran imepata mafanikio makubwa katika nyanja za teknolojia, sayansi, ulinzi na ustawi wa uchumi.
Ebenezer Oyetake mchambuzi wa masuala ya kimataifa wa nchini Nigeria amezungumza na Iran Press na kueleza kuwa Iran ni kigezo bora kwa ajili ya ustawi na kujitawala nchi zinazoendelea duniani. Bwana Ebenezer amebainisha hayo pale alipotoa ufafanuzi kuhusu uwezo wa kiulinzi na kiyasansi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na athari zake kwa diplomasia.
Mchambuzi huyo mtajika wa nchini Nigeria ameongeza kuwa vikwazo vya nchi za Magharibi vilikuwa na lengo la kuidumaza Iran hata hivyo Tehran ilibadili changamoto hiyo na kuwa nguvu kuu ya kiulinzi katika eneo.
Ebenezer Oyetake amesema, fikra za maendeleo ya Iran zinaweza kuwa mfano wa kuigwa na nchi zinazoendelea; na kwamba uwezo wa kiulinzi wa Iran umeimarisha nguvu ya makabiliano ya nchi hii dhidi ya adui.
Ebenezer ameongeza kuwa uwezo wa kiulinzi na kijeshi umeifanya Iran kuimarika pakubwa katika upande wa diplomasia kimataifa.
Mchambuzi huyo mtajika wa masuala ya kimataifa raia wa Nigeria amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imedumisha uhuru wake kwa kutumia diplomasia madhubuti, na hivi leo nchi mbalimbali zikiwemo za Kiafrika zinataka kuwa na uhusiano na Iran.
Takwimu zinaonyesha kuwa biashara kati ya Iran na nchi za Kiafrika mwanzoni mwaka mwaka huu ziliongezeka kwa asilimia 22 ikilinganishwa na mwaka uliopita.