-
Vurugu uchaguzi mdogo Kenya zaibua wasiwasi kuelekea uchaguzi mkuu 2027
Jul 18, 2026 03:30Mashambulio dhidi ya wapiga kura wakati wa uchaguzi mdogo katika eneo bunge la Ol Kalou katika mkoa wa kati nchini Kenya, yameibua hofu kuhusu hali ya usalama kuelekea uchaguzi mkuu hapo mwakani 2027.
-
Ajali mbaya ya basi la shule Uganda yaua watoto 20
Jul 17, 2026 11:41Watoto wasiopungua 20 na mtu mmoja mzima wamefariki dunia baada ya basi la shule walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika Wilaya ya Kapchorwa, mashariki mwa Uganda, polisi wamesema.
-
Ebola yazidi kuwa tishio katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Jul 17, 2026 02:57Mlipuko wa maradhi ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unasambaa zaidi ya juhudi zinazochukuliwa za kuudhibiti huku zaidi ya watu 2,000 wakiambukizwa na zaidi ya 750 wakiwa wameaga dunia.
-
Eritrea yajizatiti kukabiliana na tamaa ya Ethiopia; wasiwasi waongezeka kuhusu kurejea mvutano Pembe ya Afrika
Jul 17, 2026 02:48Dalili za kuongezeka kwa mvutano kati ya Eritrea na Ethiopia zimeibua wasiwasi wa uwezekano wa kurejea mgogoro kati ya mataifa hayo mawili ya Pembe ya Afrika.
-
Wafanyakazi wa kukabiliana na Ebola waandamana DRC wakidai mishahara yao
Jul 16, 2026 10:45Wafanyakazi wa afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameanzisha mgomo kushinikiza kulipwa mishahara na marupurupu yao ambayo hawajapokea, hatua iliyosababisha kusimama kwa shughuli za kukabiliana na virusi vya Ebola vinavyoenea kwa kasi.
-
UN: Zaidi ya watu milioni 48 Afrika Mashariki wako katika hatari ya njaa ya kutisha mwaka 2026
Jul 16, 2026 10:36Shirika la Misaada la Umoja wa Mataifa (UN) limeonya kuwa Afrika Mashariki inaendelea kuwa kitovu cha janga kubwa la kibinadamu, huku watu wapatao milioni 48.5 wakihitaji misaada ya dharura mwaka huu.
-
Umoja wa Mataifa waonya dhidi ya kutumia vibaya rasilimali za Sudan kufadhili vita
Jul 16, 2026 03:04Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba makundi yanayopigana nchini Sudan yanafaidika kutokana na udhibiti wa rasilimali za nchi hiyo, wakati uchumi wa vita ukichangia katika kuendeleza mzozo huo.
-
Kofi Annan Foundation: Yumkini Kenya ikatumbukia katika ghasia za Uchaguzi Mkuu 2027
Jul 16, 2026 02:48Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi ya Kofi Annan Foundation imeonya kuwa nchi ya Kenya iko katika hatari kubwa ya kushuhudia vurugu zinazohusiana na uchaguzi mkuu wa 2027 iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.
-
Mkuu wa wakala bandia wa serikali ya Nigeria akamatwa baada ya kuwa mafichoni kwa wiki kadhaa
Jul 15, 2026 15:36Polisi ya Nigeria imemtia mbaroni mtu aliyeanzisha wakala bandia wa serikali uliokuwa ukifanyia kazi zake katika ofisi ya Rais kwa karibu miaka miwili.
-
UN yaonya: Tishio la kigaidi linaenea kote Afrika Magharibi na Sahel
Jul 15, 2026 12:06Umoja wa Mataifa umeonya kwamba makundi ya kigaidi yanapanua wigo wao kote Afrika Magharibi na Sahel, kwa kutumia mbinu za kisasa zaidi na kutishia amani ya majimbo ya pwani katika Ghuba ya Guinea.