-
Touadera ashinda muhula wa 3 wa urais Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jan 06, 2026 02:59Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera ameshinda muhula wa tatu urais, kwa mujibu wa matokeo ya awali ya uchaguzi wa karibuni, yaliyotangazwa Jumatatu na Mamlaka ya Kitaifa ya Uchaguzi.
-
Amnesty International: Serikali ya Uganda inatumia mbinu za mateso kuwatishia wapinzani
Jan 06, 2026 00:05Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International, limetangaza kuwa, vikosi vya usalama nchini Uganda vinatumia njia za mateso na ukamataji usio wa kisheria kuwatisha wapinzani kuelekea uchaguzi mkuu katikati ya mwezi huu wa Januari.
-
Rais mteule wa Guinea: Kipaumbele changu ni kuleta umoja, utulivu na maendeleo
Jan 05, 2026 23:47Rais mteule wa Jamhuri ya Guinea, Mamady Doumbouya, ameahidi kufanyia kazi sana suala la kuleta umoja na mshikamano, utawala wa sheria na ustawi wa wananchi wote, katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
-
Jeshi la Sudan ladungua ndege zisizo na rubani za RSF, karibu 100 wameuawa Darfur ndani ya wiki moja
Jan 05, 2026 07:20Jeshi la Sudan limetangaza leo Jumatatu kwamba limedungua ndege zisizo na rubani za waasi wa Rapid Support Forces (RSF) zilizojaribu kushambulia bwawa na makao makuu ya kambi mbili za kijeshi, huku vyanzo vya matibabu vikithibitisha kwamba watu 114 wameuawa katika wiki moja katika mashambulizi tofauti katika eneo la Darfur, huko magharibi mwa Sudan.
-
Jaribio jipya la mapinduzi nchini Burkina Faso, hali inaripotiwa kuwa tete Ouagadougou, Bobo-Dioulasso
Jan 05, 2026 06:51Burkina Faso ilikumbwa na hali ya wasiwasi siku za Jumamosi na Jumapili ya jana, kufuatia ripoti za kuwepo jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais wa mpito wa nchi hiyo, Ibrahim Traoré.
-
Magaidi washambulia soko katika jimbo la Niger, Nigeria na kuuwa watu wasiopungua 50
Jan 05, 2026 04:25Polisi wa Nigeria wameripoti kuwa watu wasiopungua 50 wameuawa katika shambulio lililofanywa na magaidi wenye silaha katika soko la kijiji katika Wilaya ya Kabe, eneo la Serikali ya Mtaa ya Borgu katika Jimbo la Niger.
-
Wanamgambo wa RSF washambulia kwa droni maeneo muhimu ya Sudan
Jan 04, 2026 23:15Wanamgambo wa Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) wameshambulia vituo muhimu vya Sudan kwa kutumia ndege zisizo na rubani, na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye vituo hivyo.
-
Araghchi: Utekaji wa Rais wa Venezuela na Marekani ni mfano dhahiri wa ugaidi wa kiserikali
Jan 04, 2026 04:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelaani vikali hujuma ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela na utekaji wa Rais Nicolás Maduro pamoja na mkewe, akieleza kitendo hicho kuwa “mfano dhahiri wa ugaidi wa kiserikali” na ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya wananchi wa Venezuela.
-
Madaktari Sudan watahadharisha kuhusu maafa tarajiwa ya kibinadamu huko Kordofan Kusini
Jan 04, 2026 03:35Kundi la madakatri wa Sudan limetahadharisha kuhusu maafa tarajiwa ya kiafya na kibinadamu katika mji wa Dalang unaopatikana katika jimbo la Kordofan Kusini. Kundi hilo limesema kuwa mji wa Dalang unaendelea kuzingirwa huku ukikabiliwa na mashambulizi makali ya wanagambo wa RFS.
-
Afrika Kusini yataka UN iitishe kikao cha dharura kufuatia mashambulizi ya Marekani dhidi ya Venezuela
Jan 03, 2026 23:31Afrika Kusini imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha kikao cha dharura kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela, na kukamatwa Rais wa nchi hiyo Nicholas Maduro na mkewe.