-
Baraza la Usalama na Arab League kukutana kujadili hatua ya Israel ya kuitambua rasmi Somaliland
Dec 28, 2025 08:07Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) zimepanga kufanya mikutano tofauti wiki hii kujadili matokeo ya hatua ya Israel ya kulitambua rasmi eneo la 'Somaliland, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili.
-
Wanawake na watoto ni kati watu zaidi ya 200 waliouawa katika mauaji mapya ya kikabila huko Darfur
Dec 28, 2025 07:09Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa watu zaidi ya 200, wakiwemo wanawake na watoto wameuawa katika mashambulizi ya kikabila yaliyofanywa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) huko Darfur nchini Sudan.
-
Jamhuri ya Afrika ya Kati yaendesha uchaguzi mkuu,Touadéra anawania muhula wa tatu wa urais
Dec 28, 2025 06:52Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wameelekea kwenye masanduku ya kura katika zoezi la uchaguzi mkuu huku Rais Archange Touadéra akiwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu.
-
Somalia yaitaka Israel ifute uamuzi wake wa kuitambua Somaliland
Dec 27, 2025 23:23Somalia imeitaka Israel kubatilisha hatua yake ya kulitambua rasmi eneo la 'Somaliland, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili. Somalia imelaani hatua hiyo na kuitaja kuwa kitendo cha "uchokozi ambacho kamwe hakitavumiliwa.
-
Guinea Conakry kufanya uchaguzi wa urais wa kihistoria leo Jumapili; Mamadi Doumbouya anashiriki
Dec 27, 2025 23:22Guinea Conakry leo Jumapili inatarajiwa kufanya uchaguzi wake wa kwanza wa urais tangu baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021. Zoezi hili linayoashiria hatua muhimu katika kipindi cha uongozi wa mpito wa nchi hiyo kuelekea katika utawala wa kikatiba.
-
Ujumbe wa kwanza wa Umoja wa Mataifa wawasili El Fasher kutathmini hali ya mambo
Dec 27, 2025 07:46Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema shirika hilo limefanikiwa kupeleka ujumbe wa tathmini huko El Fasher, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan.
-
Israel yalaaniwa vikali kwa kutambua Somaliland kama nchi huru
Dec 27, 2025 03:11Utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza kutambua eneo la 'Somaliland, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili.
-
Wataalamu: Operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Nigeria inalenga kugawa taifa
Dec 27, 2025 03:10Wataalamu wametilia shaka lengo la Rais wa Marekani, Donald Trump, katika mashambulizi ya kijeshi nchini Nigeria kwa kisingizio cha kupambana na magaidi wa kundi la DAESH (ISIS/ISIL) kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
-
Waziri Mkuu wa Sudan akataa vikosi vya kimataifa, akubali uangalizi wa masharti
Dec 27, 2025 03:09Waziri Mkuu wa Sudan, Kamil Idris, alisema Ijumaa kwamba serikali ya nchi hiyo haitakubali kupelekwa kwa vikosi vya kimataifa katika mchakato wowote wa amani ujao, ingawa imekubali uwepo wa uangalizi kwa masharti.
-
Yemen yasema iko tayari kwa vita, yawataka Waislamu wawe macho
Dec 27, 2025 03:08Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen amesema taifa hilo linaendelea kujiandaa usiku na mchana kwa duru ijayo ya vita visivyoweza kuepukika dhidi ya Marekani na Israel, akiahidi kuwa harakati za Muqawama au mapambano ya Kiislamu za Kiyemeni hazitasimamishwa wala kupokonywa silaha.