-
Serikali ya Ethiopia yashtakiwa kwa kuwatelekeza wakimbizi
Dec 26, 2025 23:16Shirika la Kutetea Haki za Binadamu nchini Ethiopia, la Human Rights First limeishtaki serikali ya Ethiopiia kwa kile lilichodai hatua ya serikali ya Addis Ababa ya kuwatelekeza wakimbizi.
-
Umoja wa Mataifa waisihi Guinea kukomesha ukiukwaji wa haki kabla ya uchaguzi
Dec 27, 2025 03:11Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ameitaka serikali ya Guinea kukomesha mara moja vitendo vya vitisho na ukiukwaji wa haki za binadamu kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika kesho Jumapili tarehe 28 Desemba, akionya kuwa hali ya sasa inahatarisha uhalali wa mchakato wa uchaguzi.
-
UN yatahadharisha: Al-Shabab bado ni tishio kubwa nchini Somalia na Kenya
Dec 26, 2025 08:24Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wametahadrharishakatika ripoti yao wiki hii kwamba kundi lenye misimamo mikali la al Shabab lingali ni tishio kubwa hivi sasa kwa amani na uthabiti huko Somalia na katika eneo zima pa Pembe ya Afrika ikiwa ni pamoja na katika nchi jirani ya Kenya.
-
Polisi wa Zambia apongezwa kwa kukataa hongo ya $50,000 kwenye uwanja wa ndege wa Lusaka
Dec 26, 2025 02:44Tume ya Kupambana na Rushwa ya Zambia (ACC) imempongeza askari polisi wa kike aliyekataa kupokea hongo ya dola za Kimarekani 50,000 kutoka kwa mshukiwa wa utakatishaji pesa katika uwanja wa ndege wa mji mkuu wa nchi hiyo, Lusaka.
-
UN yalaani vikali shambulio la kigaidi lililoua waumini msikitini jimboni Borno, Nigeria
Dec 25, 2025 23:53Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea kwenye msikiti ulioko katika Soko la Gamboru, mjini Maiduguri, katika Jimbo la Borno kaskazini-mashariki mwa Nigeria, lililopelekea kuuawa na kujeruhiwa makumi ya Waislamu waliokuwemo msikitini humo.
-
Sudan katika ukingo wa shimo la maangamizi, RSF washadidisha mashambulizi
Dec 25, 2025 23:33Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF nchini Sudan vimetangaza kwamba vimezidisha mashambulizi na kuchukua udhibiti wa maeneo ya Abu Qamra na Ombro katika jimbo la Darfur Kaskazini, huko magharibi mwa Sudan.
-
Uchaguzi wa moja kwa moja Somalia kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya nusu karne
Dec 25, 2025 08:19Wakazi wa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa baraza la mitaa, tukio la kihistoria kwani ni mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 50 wananchi kuchagua wawakilishi wao moja kwa moja. Hata hivyo, hatua hii imegubikwa na upinzani wa vyama vilivyokataa kushiriki.
-
Guterres atoa wito wa uchaguzi wa amani na jumuishi CAR
Dec 25, 2025 08:17Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa raia wote wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa nchi hiyo, akisisitiza umuhimu wa utulivu, nidhamu na kuheshimu misingi ya kidemokrasia kabla ya uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 28 Desemba.
-
40 wauawa, kujeruhiwa katika shambulio la bomu Msikitini Maiduguri, Nigeria
Dec 25, 2025 02:13Mripuko mkubwa wa bomu umeripotiwa kutikisa Msikiti mmoja wakati wa Swala ya Magharibi usiku wa kuamkia leo huko mjini Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
Bunge la Algeria laidhinisha sheria inayojinaisha ukoloni wa Ufaransa
Dec 25, 2025 00:03Bunge la Algeria jana Jumatano lilipasisha kwa kauli moja sheria inayotambua ukoloni wa Ufaransa nchini humo kuwa ni jinai, ikiutaja kuwa ni "uhalifu wa serikali," na kuitaka Ufaransa iombe msamaha rasmi kwa jinai hiyo.