-
Israel yazingirwa majini na nchi tajiri zaidi ya Kiarabu kwa mtazamo wa ujasiri na heshima
Dec 17, 2023 04:26'Sasa kwa vile chakula na dawa vimezuiwa kuingia Gaza, tutazuia meli kuingia na kutoka Tel Aviv.' Hayo ni matamshi yalitolewa na Brigedia Jenerali Yahya Saree, Msemaji rasmi wa Jeshi la Yemen, na hii ina maana kwamba Yemen italenga meli zote zinazoelekea Tel Aviv bila kubagua ni meli ya nchi gani.
-
Kushindwa Umoja wa Ulaya kuchukua msimamo wa pamoja kuhusu mgogoro wa vita vya Gaza
Dec 16, 2023 08:03Mkutano wa siku mbili wa Baraza la Ulaya umemalizika huku viongozi wa nchi 27 za Ulaya wakishindwa kufikia makubaliano ya pamoja katika taarifa yao ya mwisho kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na matukio ya Gaza.
-
Droni Karrar yenye kombora Majid, mafanikio muhimu ya ulinzi wa anga wa Jeshi la Iran
Dec 16, 2023 03:23Siku chache zilizopita mamia ya ndege zisizo na rubani (droni) aina ya Karrar zilizo na makombora yanayojulikana kwa jina Majid, ziliongezwa katika Kikosi cha Ulinzi wa Anga katika maeneo yote ya mipakani ya Iran.
-
Waziri wa Mambo ya Nje waTaliban asisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano na Iran
Dec 15, 2023 23:22Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa serikali ya Taliban ya Afghanistan amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kudumisha na kuimarisha uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kufutwa Hamas; lengo lisiloweza kufikiwa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza
Dec 15, 2023 04:13Huu ni mwezi wa tatu tangu utawala ghasibu wa Israel uanzishe vita vya kikatili dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza lakini pamoja na hayo umeshindwa kabisa kufikia malengo ya kijeshi uliyoyatangaza rasmi kabla ya kuanzisha vita hivyo likiwemo la kuangamiza Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina, Hamas.
-
Kuidhinishwa kuanza rasmi uchunguzi wa kumsaili Biden katika Bunge la Wawakilishi la Marekani
Dec 14, 2023 23:26Bunge la wawakilishi la Marekani jana Jumatano lilipasisha azimio kwa kura 221 za ndio mkabala wa 212 za kupinga kuanzisha rasmi uchunguzi wa kumsaili Rais Joe Biden wa nchi hiyo. Kabla ya kura hiyo, Kelly Armstrong, Mwakilishi wa Kongresi ya Marekani kwa niaba ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, alichapisha rasimu ya azimio kwa ajili ya kuendelea uchunguzi huo tajwa kwa lengo la kumuuzulu Rais Joe Biden wa Marekani.
-
Iran; Mwenyeji wa idadi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani
Dec 14, 2023 08:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika Kongamano la Baraza la Wakimbizi Duniani huko Geneva Uswisi kwamba: 'Nataraji kuwa Umoja wa Mataifa na Kamisheni Kuu ya Wakimbizi Duniani zitatekeleza majukumu yao kuhusu wakimbzi na hasa kuhusu raia wa Kiafghani milioni tano wanaoishi Iran.'
-
Kutokuwa na nia nchi za Magharibi kuipa Uturuki uanachama katika Umoja wa Ulaya
Dec 14, 2023 03:38Huku serikali ya Uturuki ikiwa imeanzisha juhudi mpya za kujiunga na Umoja wa Ulaya, matokeo ya kura mpya ya maoni yanaonyesha kuwa raia wengi wa Ulaya wanapinga nchi hiyo kupewa uanachama katika umoja huo.
-
Vita vya kimtandao sambamba na vita vya kijeshi dhidi ya utawala wa Kizayuni
Dec 13, 2023 07:06Utawala wa Kizayuni ambao haujapata mafanikio yoyote katika vita vya kijeshi dhidi ya Wapalestina, umekabiliwa na vita vikubwa vya mitandao ya kijamii.
-
Hali ya zama za mwisho ya Ukanda wa Gaza
Dec 13, 2023 03:39Mashambulizi makali ya ndege za kivita ya jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza yaliendelea jana Jumanne kwa masaa kadhaa.