-
Ukurasa mwingine wa maafa ya binadamu huko Yemen; wagonjwa elfu tano wanaohitaji huduma ya Dialysis wanakaribia kuaga dunia
Jan 16, 2023 23:21Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen Anayehusika na Masula ya Tiba ameeleza kuwa maisha ya wagonjwa elfu tano wenye matatizo ya figo wako kwenye hatari ya kifo na Umoja wa mataifa na jamii ya kimataifa ndizo zinazopaswa kubeba dhima ya uhai na maisha ya raia hao wa Yemen.
-
Maandamano ya mapema dhidi ya serikali ya Netanyahu; indhari kuhusu vita vya ndani
Jan 16, 2023 04:46Makumi ya maelfu ya wakazi wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel) wameandamana kulalamikia maamuzi yaliyochukuliwa na serikali ya Benjamin Netanyahu ya kubana mfumo wa mahakama wa utawala huo.
-
Indhari ya Evo Morales kuhusu nia ya Marekani ya kufanya mapinduzi Amerika ya Latini
Jan 15, 2023 22:56Evo Morales, Rais wa zamani wa Bolivia amesema kuwa, Marekani ipo katika mkondo wa kuporonmoka hasa kwa kuzingaia matukio ya hivi karibuni katika baadhi ya mataifa ya Amerika ya Latini na ni kutokana na sababu hiyo ndio maana Washington imeamua kutumia mabavu na kwamba, hivi sasa inatekeleza njama za mapinduzi katika maeneo ya Ukanda huo.
-
Radiamali hasi ya Madola ya Magharibi ya kunyongwa jasusi wa Uingereza nchini Iran
Jan 15, 2023 08:13Kunyongwa Ali Reza Akbari, jasusi wa shirika la kijasusi la Uingereza la MI6 kumekabiliwa na matamshi ya pupa na radiamali tofauti na hasi za madola ya Magharibi. Radiamali hizo zinaonyesha kupata pigo kubwa mipango ya kijasusi ya Magharibi dhidi ya Iran.
-
Sababu za umuhimu wa safari ya Amir-Abdollahian nchini Lebanon
Jan 14, 2023 22:52Hossein Amirabdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kuzungumza na Abdallah Bou Habib, Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Lebanon katika safari yake mjini Beirut na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima itaendelea kuwa rafiki mwaminifu na wa kutegemewa wa Lebanon.
-
Siasa za upande mmoja za Marekani dhidi ya Iran; kudhoofishwa utawala wa sheria na kukiukwa Hati ya Umoja wa Mataifa
Jan 14, 2023 03:32Akizungumza Alkhamisi katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichofanyika chini ya anwani "Kukuza na Kuboresha Utawala wa Sheria katika Kudumisha Amani na Usalama wa kimataifa" Amir Saeed Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika umoja huo amesema kwamba hatua zisizo za kisheria na za upande mmoja za Marekani dhidi ya nchi huru wanachama wa Umoja wa Mataifa, kama vile Iran, zinadhoofisha utawala wa sheria na kukiuka Hati ya umoja huo.
-
Maonyo ya kimataifa kuhusu ukame mkali nchini Afghanistan
Jan 14, 2023 00:21Maonyo makali ya kimataifa yametolewa kuhusu ukame mkali unaotokana na kushadidi baridi na kuongezeka mgogoro wa kiuchumi nchini Afghanistan. Jamii ya kimataifa inasisitiza kuwa, iwapo hali ya hivi sasa itaendelea, basi wananchi milioni 6 wa Afghanistan watakumbwa na ukame wa kuchupa mipaka.
-
Mahesabu mabovu ya maadui kuhusu nguvu za irada na azma ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Jan 13, 2023 10:48Maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran walitumia uwezo na nguvu zao zote katika machafuko ya hivi karibu kujaribu kutoa pigo kwa Iran ya Kiislamu, lakini kama ilivyojiri kwa miaka ya huko nyuma, njama zao za mara hii pia zimesambaratika na kwa mara nyingine umoja na mshikamano wa wananchi pamoja na nguvu na uimara wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umefelisha njama hizo.
-
Kushtadi mashinikizo ya Ukraine kwa wapinzani kwa kuwavua uraia wanaoipinga serikali ya Zelenskyy
Jan 12, 2023 23:34Nchi za Magharibi, kinyume na nara na kaulimbiu zao za kizandiki za kutetea utu na ahadi zao za kusimamia kidemokrasia, zimeshakiuka mara nyingi misingi hiyo; na sio tu haziwezi kuwavumilia wapinzani na wakosoaji wao, bali hutumia pia njia mbalimbali kuzima sauti zao au hata kuwamaliza moja kwa moja.
-
Mpango wa Kikosi cha Wanamaji cha Kimkakati cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuwepo katika maji ya kimataifa
Jan 12, 2023 05:34Admeri Shahram Irani, Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi amesema: "leo kutumia fursa za bahari ni jambo lenye manufaa ya kijiopolitiki kwetu sisi; na wale wasio na uwezo wa kufanya hivyo wanashindwa kupumua kijiopolitiki".