Feb 09, 2023 02:43 UTC
  • UNICEF yaonya kuhusu hali mbaya ya binadamu nchini Afghanistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetahadharisha kuhusu matokeo mabaya ya kushadidi mgogoro wa binadamu nchini Afghanistan.

UNICEF imezitaka jumuiya za kimataifa kutoisahau Afghanistan. Onyo hili ni muhimu sana kwa kuzingatia msimu wa baridi kali, ambao wakati mwingine huwa wa aina yake katika historia ya Afghanistan. 

Inaonekana kwamba masuala mawili yamekuwa na taathira katika mwenendo wa sasa wa jamii ya kimataifa wa kupuuza matatizo ya Afghanistan hasa katika mwaka mmoja na nusu uliopita kwa uchache. Kwanza ni matukio ya kisiasa ya nchi hiyo na kurejea madarakani kundi la Taliban. Kutotambuliwa rasmi utawala wa Taliban na jamii ya kimataifa kumepunguza mawasiliano ya kimataifa na kundi hilo. Hasa kwa kutilia maanani kwamba hatua za hivi karibuni za Taliban za kuzuia wasichana wa Kiafghani kupata elimu ya chuo kikuu na marufuku ya wanawake kufanya kazi katika makampuni binafsi na taasisi za kimataifa vimezivunja moyo jumuiya za kikanda na kimataifa. Abdulatif Nazari, mhadhiri wa chuo kikuu nchini Afghanistan, anasema: "Watu wa Afghanistan wako katika hali mbaya sana ya kimaisha na msimu wa baridi kali umezidisha matatizo yao. Katika hali hii, jumuiya za kimataifa, ambazo zimekatishwa tamaa na hali ya kisiasa ya Afghanistan hazipaswi kuwaacha watu wa nchi hii peke yao. Kwa sababu Waafgani hawawezi tena kustahimili mashinikizo yalilosababishwa na miongo miwili ya vita na uvamizii wa Marekani na washirika wake." 

Watoto wa Afghanistan

Sababu ya pili inayozifanya jumuiya za kimataifa zipuuze matatizo ya Afghanistan ni mzozo wa Ukraine. Kwa kujiondoa Afghanistan na kuchochea vita huko Ukraine, kwa hakika Marekani ilielekeza mazingatio ya ulimwengu katika upande huo. Tunasisitiza kuwa juhudi za Marekani za kutafuta waitifaki dhidi ya Russia zimeelekkeza mazingatio ya walimwengu kwenye mgogoro wa Ukraine na kuwafanya wasahauu mgogoro wa Afghanistan na matatizo ya watu wa nchi hiyo. Hii ni licha ya kwamba, sababu kuu ya matatizo ya watu wa Afghanistan ni Marekani na nchi nyingine za Magharibi, ambazo zimeibua mgogoro wa Ukraine kwa mujibu wa maslahi yao haramu na kuwaacha watu wa Afghanistan pekee yao katika msimu wa baridi kali.

Soroush Amiri, mtaalamu wa masuala ya Afghanistan, anasema: "Marekani imefanya uhalifu mkubwa dhidi ya watu wa Afghanistan kwa kunyakua takriban dola bilioni kumi mali ya Waafghani. Marekani ambayo iliivamia na kuikalia kwa mabavu Afghanistan kwa miongo miwili, iliharibu miundombinu yote ya kiuchumi ya nchi hiyo; na baada ya miongo miwili, ilikabidhi nchi iliyoharibiwa kwa watu wa Afghanistan, ambao bado wanateseka."

Askari vamizi wa Marekani nchini Afghanistan

Kwa vyovyote vile, tahadhari ya UNICEF na mashirika mengine ya kimataifa kuhusu kuzorota kwa hali ya kiuchumi ya Afghanistan ina umuhimu mkubwa na inaweza kuvutia mazingatio ya kimataifa katika kadhia hii. Hata hivyo haionekani kuwa tahadhari hiyo itaamsha dhamiri zilizolala za duru za Kigharibi hasa Marekani ambayo ndio sababu ya kuangamizwa na kuharibiwa Afghanistan. Pamoja na hayo kundi la Taliban pia lina jukumu zito katika kesi hii, na kama mtawala wa Afghanistan, linapaswa kufanya jtihada zaidi kwa ajili ya kuelekeza mazingatuo ya kimataifa kwa hali ya watu wa nchi hiyo.

Sambamba na hayo Umoja wa Mataifa haupaswi kutosheka na maonyo kama haya, bali pamoja na hayo, unapaswa kutumia suhula zake zote na kuwa na nafasi muhimu na yenye taathira katika kutatua matatizo ya watu wa Afghanistan.

Tags