-
Kuongezeka mpasuko na utesi wa kisiasa katika serikali tete ya utawala wa Kizayuni
Dec 09, 2021 06:19Mamia ya wakati wa Tel-Aviv, makao makuu ya utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya maandamano ya kupinga serikali ya nchi hiyo wakishinikiza kujiuzulu waziri mkuu Naftali Bennett na kutaka arejee madarakani Benjamin Netanyahu.
-
Marekani yasusia kidiplomasia michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi nchini China
Dec 09, 2021 01:14Jen Psaki Msemaji wa Ikulu ya White House alitangaza Jumatatu usiku kuwa, "serikali ya Joe Biden haitatuma mwakilishi rasmi au wa kidiplomasia katika michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi." Amedai kuwa sababu ya uamuzi huo wa serikali ya Marekani ni mauaji ya kimbari na jinai dhidi ya binadamu katika mkoa wa Xinjiang na vitendo vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu China.
-
Kuhukumiwa kifungo cha miaka minne jela Aung San Suu Kyi
Dec 07, 2021 23:03Mahakama nchini Myanmar imemhukumu kifungo cha miaka minne jela Aung San Suu Kyi kiongozi wa kilichokuwa chama tawala nchini humo cha National League for Democracy (NLD).
-
Hatua za Imarati za kuboresha uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Dec 07, 2021 04:32Jumatatu ya jana ya tarehe 6 Disemba, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) alifanya safari ya siku moja hapa mjini Tehran ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwemo Rais Sayyid Ibrahim Raeisi na Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa.
-
Tahadhari iliyotolewa na Algeria kuhusu njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kulidhibiti bara la Afrika
Dec 07, 2021 01:26Kwa muda mrefu sasa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umetumia sera na mbinu tofauti ili kujipenyeza na kuwa na satua katika nchi za Afrika, muhimu zaidi ikiwa ni ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na nchi za Kiarabu; sera ambayo imeweza kutekelezwa kivitendo katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita kwa msaada na uungaji mkono wa Marekani.
-
Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria mjini Tehran
Dec 06, 2021 05:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Faisal al Miqdad ambaye jana usiku aliwasili hapa mjini Tehran, leo Jumatatu, tarehe 6 Desemba amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian, ambapo wawili hao wamejadili na kubadilishana mawazo juu ya masuala mbali mbali yanayohusu pande mbili.
-
Mazungumzo ya Vienna yakisubiri maamuzi ya maana na ya kimantiki
Dec 05, 2021 22:54Mazungumzo yanayohusiana na kuondolewa vikwazo vya kidhulma vya Marekani dhidi ya Iran, yalianza Jumatatu ya wiki iliyopita mjini Vienna, Austria. Siku ya Ijumaa mazungumzo hayo yalisimamishwa kwa muda ili kutoa fursa kwa washiriki kurejea katika nchi zao kwa mashauriano.
-
Onyo kuhusu hatari ya kupata nguvu tena genge la Daesh eneo la Kurdistan nchini Iraq
Dec 05, 2021 07:33Mkuu wa chama cha Democrat cha eneo la Kurdistan la Iraq na ambaye pia ni rais wa serikali ya ndani ya eneo hilo ameonya kuhusu hatari ya kupata nguvu upya genge la Daesh (ISIS) kwenye eneo hilo.
-
Marekani yaendelea kushirikiana na Saudi Arabia katika vita vya Yemen
Dec 04, 2021 23:07Mashambulio ya mabomu dhidi ya Yemen yanayofanywa na jeshi la muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yanaendelea huku nchi za Magharibi, zinazotoa nara za kutetea haki za binadamu hususan Marekani, zikiendelea kuisaidia Saudi Arabia katika kutenda jinai dhidi ya wananchi wa Yemen.
-
Kuongezeka kwa mzozo kati ya Russia na Magharibi juu ya Ukraine na upanuzi wa NATO kuelekea Mashariki
Dec 04, 2021 11:06Katika wiki za hivi karibuni, makabiliano kati ya Russia na Magharibi kuhusu Ukraine yamechukua sura mpya, huku pande mbili zikitoa maonyo ya mara kwa mara kuhusu hatua zozote za kijeshi.