Jan 12, 2024 10:35
Msemaji wa majeshi ya Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Sarii amesema kuwa, mashambulizi ya kiuadui ya Marekani na Uingereza hayatobadilisha msimamo wa Yemen wa kuliunga mkono taifa la Palestina ikiwemo Ghaza na kwamba uadui huo uliofanyika mapema leo Ijumaa dhidi ya Yemen hautoachwa vivi hivi bila ya majibu na kuadhibiwa madola hayo ya kibeberu.