-
Kumbukumbu ya siku aliyofariki dunia Bwana Mtume Muhammad SAW + Sauti
Oct 28, 2019 01:47Katika kumbukumbu ya kifo cha Bwana Mtume Muhammad SAW nchini Tanzania, viongozi wa dini ya Kiislamu wametakiwa kuweka mikakati imara ya kuwalingania vijana na sio kuwaona ni waasi waliopotoka. Amari Dachi na taarifa zaidi akiripoti kutoka Dar es Salaam.
-
Televisheni ya Iraq yarusha hewani video ya shambulio lililomuua mkuu wa ISIS + Video
Oct 27, 2019 08:49Televisheni ya serikali ya Iraq imerusha hewani mkanda wa video na kusema kuwa ni shambulio lililopelekea kuuawa kiongozi wa genge la kigaidi la Daesh (ISIS), Abu Bakr al Baghdadi.
-
SAUTI, Rais Faustin Touadéra wa CAR aitaka Russia kulinoa kila upande jeshi la nchi yake, aamua kuachana na Wamagharibi
Oct 25, 2019 12:31Rais Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ametetea mpango wake wa kupanua ushirikiano zaidi wa kijeshi, kisiasa na kiuchumi kati ya nchi yake na Russia.
-
SAUTI, Rais Museven wa Uganda: Russia ilizisaidia sana nchi za Afrika kudai uhuru wao, hivyo iendeleze roho hiyo
Oct 25, 2019 12:30Rais Yoweri Museven wa Uganda ameitaka Russia kupanua zaidi ushirikiano wake na mataifa ya Afrika huku akiipongeza nchi hiyo kutokana na juhudi zake za kusaidia harakati za kujikomboa za nchi za bara hilo.
-
SAUTI, Mahakama ya Tanzania yapigilia msumari sheria ya ndoa ya utotoni, yataka binti aliye chini ya miaka 18 asiolewe
Oct 24, 2019 13:47Mahkama ya Rufaa nchini Tanzania imeitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kubadili vifungu vya sharia ya ndoa vinavyomruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18 kwa lengo la kutoa usawa baina ya mtoto wakike na wakiume.
-
SAUTI, Idadi ya wa wagonjwa wa ukoma inazidi kuongezeka nchini Burundi, wananchi watakiwa kupima afya mapema
Oct 24, 2019 13:27Wagonjwa wa maradhi ya ukoma wametajwa kuongezeka nchini Burundi, licha ya serikali ya nchi hiyo kutokuwa na idadi kamili ya wagonjwa hao.
-
SAUTI, Serikali ya Kenya: Hadi sasa watu 29 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko ya mvua zinazonyesha nchini
Oct 24, 2019 13:24Serikali ya Kenya imethibitisha kufariki dunia watu 29 kutokana na mafuriko yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.
-
Kenya yaomba msaada wa UN kupambana na majangili + Sauti
Oct 24, 2019 04:07Kenya imesalimu amri na kuuomba Umoja wa Mataifa uisaidie kukabiliana na biashara za uwindaji haramu. Serikali ya Kenya imesema, licha ya juhudi zake za kupambana na ujangili, lakini bado kazi ni pevu na inahitajia msaada wa kimataifa. Mwandishi wetu Seifullah Murtadha na maelezo zaidi kutoka Mombasa, Kenya.
-
SAUTI, Dunia yaombwa kusaidia kuzima mauaji ya Banyindu, Bafurero, Wabembe nk Kivu Kusini, Kongo DR
Oct 22, 2019 13:17Jamii ya kimataifa imetakiwa kusaidia kuhitimisha mapigano ya wenyewe kwa wenye yaliyoanza mwanzoni mwa mwaka huu katika maeneo ya nyanda za juu mkoa wa Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kupelekea kwa akali watu 500 kuuawa.
-
SAUTI, Rais Félix Tshisekedi aanzisha mchakato shirikishi wa kurejesha usalama mashariki mwa Kongo DR
Oct 19, 2019 10:51Rais Félix Antoine Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameanzisha mazungumzo na marais wa Rwanda na Uganda kwa lengo la kuwarejesha nchini waazi wa M23 waliokimbilia nchi hizo hapo mwaka 2013.