-
Zoezi la uandikishaji vitambulisho vya Mzanzibari Mkazi lakumbwa na malalamiko + Sauti
Oct 02, 2018 07:34Zoezi la kusajili vitambulisho vya Mzanzibari Mkazi limekamilika katika mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja na hivi sasa linaendelea katika mkoa wa mjini Magharibi. Hata hivyo usajili huo umegubikwa na malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaodai kwamba licha ya kuwa na haki ya kusajiliwa lakini wananyimwa haki yao hiyo. Harith Subeit ametutayarishia ripoti maalumu kuhusu suala hilo...
-
Burundi waadhimisha Siku ya Makazi Dunia + Sauti
Oct 02, 2018 07:05Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya makazi, nchini Burundi siku hiyo imeadhimishwa kwa kuhamasisha raia kukabiliana na takataka zinazotoka majumbani. Mwandishi wetu Hamida Issa na maelezo zaidi...
-
UNESCO yasikitishwa na uchache wa urithi wa kihistoria barani Afrika ulioorodheshwa kwa shirika hilo + Sauti
Oct 02, 2018 06:58Wanahistoria na wasajili wa mambo ya kale wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamadunia (UNESCO) wamesikitishwa na uchache wa alama za kihistoria barani Afrika uliopo kwenye shirika hilo. Wataalamu hao ambao wametembelea Kigali nchini Rwanda wamesema kuwa asilimia 85 ya alama za kihistoria katika shirika hilo si za Afrika. Silvanus Karemera na ripoti kamili kutoka Kigali...
-
Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania: Watanzania wanaoishi mpakani wasisumbuliwe na vyombo vya usalama
Oct 01, 2018 01:37Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Alphaxard Kangi Ndege Lugola amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo kutowasumbua Watanzania wanaoishi mipakani lakini wakati huo huo wawatie mbaroni raia wa kigeni walioingia nchini humo kinyume cha sheria. Ammar Dachi ametuyarishia ripoti maalumu kuhusu suala hilo...
-
Iran yashambulia kwa makombora makao ya viongozi wa jinai za Ahvaz + Video
Oct 01, 2018 00:06Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limeshambulia kwa makombora makao ya wakuu wa genge la kigaidi lililohusika katika mashambulizi ya kiholela yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Ahvaz wa kusini magharibi mwa Iran.
-
Ibrahim al-Jaafari: Madai ya Netanyahu juu ya uwepo wa askari wa Iran nchini Iraq ni uongo mtupu + Video
Sep 29, 2018 11:43Ibrahim al-Jaafari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq ametupilia mbali madai yasiyo na msingi wowote ya Waziri Mkuu wa utawala Haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu juu ya uwepo wa askari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Iraq na kuongeza kuwa, maneno hayo ni uongo mtupu.
-
Burundi yashauriwa kujitoa katika Baraza la Haki za Binadamu la UN + Sauti
Sep 28, 2018 02:56Baada ya serikali ya Burundi kujiondoa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo yameitaka serikali ya Bujumbura kujiondoa pia kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.
-
SAUTI, Serikali ya Uganda yagawa fedha kwa vijana wa mitaani ili kuwashawishi wasifuate mkumbo wa siasa
Sep 24, 2018 12:55Serikali ya Uganda chini ya Rais Museven imeanzisha kampeni kugawa fedha za mkopo wa riba nafuu kwa vijana sambamba na kuwataka wasishawishiwe na kimbunga kipya cha kisiasa nchini.
-
Wanafunzi wenye ulemavu walalamikia changamoto zinazowakumba Zanzibar + Sauti
Sep 23, 2018 13:43Wanafunzi wenye ulemavu visiwani Zanzibar wamelalamikia changamoto wanazozipata wakati wanapokwenda mashuleni kutokana na kukosekana miundimbinu iliyo rafiki kwao. Mwandishi wetu Harith Subeit na ripoti kamili
-
Waziri Mkuu wa Tanzania aongoza maziko ya wahanga wa ajali ya MV Nyerere + Sauti
Sep 23, 2018 13:22Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ameongoza mazishi ya kitaifa ya watu tisa kati ya 224 waliofariki kwenye ajali ya Kivuko cha MV Nyerere katika ziwa Victoria Septemba 20, 2018 ambao wamezikwa katika viwanja vya shule ya Sekondari Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza. Kati ya watu hao tisa, miili ya watu wanne ni ile ambayo haikutambuliwa. Mwandishi wetu wa Dar es Salaam Ammar Dachi anatutaarifu zaidi.