Sep 05, 2023 07:00 UTC
  • Mabinti wa Iran watwaa ubingwa wa Asia wa mchezo wa Taekwondo

Duru ya 12 ya Mashindano ya Vijana ya Taekwondo nchini Lebanon ilimalizika Jumatatu kwa timu ya mabinti ya Iran kutwaa taji la ubingwa wa Asia.

Baada ya siku 3 za mchuano wa mkali katika duru ya 12 ya mashindano ya Vijana ya Taekwondo ya Asia, wasichana wa Iran wameliwekea heshima taifa la katika bara la Asia baada ya kuwa mabingwa huku kaka zao wakishika nafasi ya tatu kwa upande wa wavulana.

Wachezaji 285 wa taekwondo kutoka nchi 26 walishiriki katika mashindano hayo yaliyofunga pazia lake hapo jana. Mashindano hayo yalikuwa yakifanyika katika Uwanja wa Michezo wa Ndani wa Nouhad Naufal huko Beirut mji mkuu wa Lebanon.

Timu ya wasichana ya Iran imeibuka kidedea baada ya kuzoa medali 9, zikiwemo dhahabu 6, fedha 2 na shaba 1. Timu ya wanawake ya Thailand ilishika nafasi ya pili huku mabinti kutoka Korea Kusini wakiambulia nafasi nafasi ya tatu katika mashindano hayo.

Tags