Rais wa Iran: Maadui hawatafanikiwa kamwe kupotosha ukweli wa Qur'ani
Sep 20, 2023 08:02 UTC
Rais Ebrahim Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa Iran amelihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kueleza kwamba, maadui hawatafanikiwa kupotosha uhakiika wa Qur'ani.
Rais wa Iran ameyanyua juuu kiitabu cha Qur'an na kuwapa ujumbe walimwengui kwa kusema: "Qur'an hii ni yenye mafunzo adhimu sana, ni Kitabu kinachotengeneza utamaduni mzuri wa Mwanadamu, ni Kitabu Kitukufu kinachomtengeneza vyema Mwanadamu, ni kitabu chenye kutengeneza jamii ya mwanadamu, ni kitabu cha milele, na kuupotosha ukweli wa Qur'an ni kitu ambacho hakiwezekani, hii Qur'an huwezi kuichoma moto na kuipoteza abadan"...