Oct 06, 2023 07:50 UTC
  • Qalibaf aendelea na mashauriano huko Abu Dhabi; akutana na Rais wa Imarati

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kuhusu kustawisha uhusiano wa pande mbili.

Katika mazungumzo hayo, Muhammad Bagher Qalibaf ameashiria kipaumbele cha awali cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa sera zake za nje kuwa ni kuwasiliana na nchi jirani na kueleza kuwa, katika uwanja huo, kustawisha uhusiano wa kiuchumi, kisaisa na kudumisha usalama endelevu baina ya nchi jirani khususan nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi ni suala lenye umuhimu mkubwa.  

Qalibaf ameitaja ziara yake nchini Imarati kuwa ni ishara ya azma thabiti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kustawisha uhusiano na kwamba ni fursa ya kutathmini yaliyopita na kuongeza kuwa: Iran inakusudia kutekeleza hatua madhubuti kati nyanja zote kwa ajili ya siku za usoni ili kustawisha uchumi wa nchi mbili katika nyuga zote ambapo kuna fursa nyingi katika uwanja huo. 

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hamu na mwaliko wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa Rais wa Imarati kwa ajili ya kuitembelea Iran na kueleza kuwa: Ni suala muhimu kustawisha uhusiano hasa katika nyanja za kiuchumi na kiusalama, na hili lina umuhimu mkubwa kwa kuzingatia hali ya kieneo, EURASIA na BRICS ambapo nchi mbili hizi hivi karibuni zimekuwa wanachama katika jumuiya hiyo. 

Wanachama wapya wa BRICS 

Sheikh Muhammad bin Zayid al Nahyan Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) pia ameashiria katika mazungumzo hayo kuhusu uhusiano wa siku nyingi wa nchi mbili za Iran na Imarati na akasema: Wakati mwingine hali ya kimataifa hupelekea kujiweka mbali nchi mbalimbali na hivyo upo ulazima wa kutafuta njia ya kukurubiana zaidi pande mbili ambapo kutumwa Balozi mpya wa Iran huko Abu Dhabi kunatoa msukumo zaidi wa kupanuliwa  uhusiano baina ya nchi mbili. 

 

Tags