Oct 12, 2023 13:30 UTC
  • Spika wa Iran azungumza na maspika wa nchi 7 za Kiislamu kuhusu jinai za Wazayuni Palestina

Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Iran) amefanya mazungumzo ya simu kwa nyakati tofauti na maspika wa mabunge ya nchi za Kiislamu za Uturuki, Algeria, Syria, Imarati, Lebanon, Oman na Kuwait na kuwahimiza wajibu wa kuchukuliwa hatua za haraka za kukomesha jinai za Wazayuni katika Ukanda wa Ghaza huko Palesitna.

Baada ya wanamapambano wa Palestina kufanya operesheni ya kishujaa na ya kihistoria Jumamosi wiki hii ya tarehe 7 Oktoba waliyoipa jina la #Kimbunga_cha_al-Aqsa, utawala wa Kizayuni umeamua kuonesha zaidi sura yake ya kijinai kwa kuwashambulia kiwendawazimu na kikatili mno wananchi wa Palestina. 

Wizara ya Afya ya Palestina imesema kuwa, zaidi ya Wapalestina 1,345 wameshauawa shahidi na zaidi ya 5,000 wengine wamejeruhiwa tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha jinai zake dhidi ya watoto, wanawake na raia wa Palestina.

Mohammad Bagher Ghalibaf, Spika wa Bunge la Iran amewashauri maspika wenzake wa nchi hizo saba za Kiislamu kuitisha kikao cha dharura cha mabunge ya nchi za Kiislamu kwa njia ya Intaneti, ili kujadiliana njia za kukomesha mashambulio ya kijinai ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Ghaza. 

Wazayuni wamezidisha jinai zao dhidi ya maeneo ya raia ya Wapalestina

 

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, katika mazungumzo yake hayo ya nyakati tofauti, Spika wa Bunge la Iran ameelezea kusikishwa sana na jinsi Israel inavyofanya jinai dhidi ya wanawake na watoto wa Palesitna na kusisitizia haja ya kuchukuliwa hatua madhubuti kimataifa za kuadhibiwa Wazayuni watenda jinai. 

Vile vile ametaka kukomeshwa mara moja mashambulio ya kijinai ya Israel dhidi ya maeneo ya raia huko Ghaza na nchi za Kiislamu zishirikiane kuwapelekea misaada wananchi madhlumu wa Palestina hasa wa Ukanda wa Ghaza.

Ikumbukwe kuwa utawala wa Kizayuni umeuzingira kila upande Ukanda wa Ghaza kwa miaka mingi na hivi sasa umewakatia maji, umeme na njia zote za kuingia na kutoka na umepiga marufuku kufikishiwa chakula, madawa na mahitaji ya dharura wananchi wa Ghaza.  

Tags