Iran imefanikiwa kutuma chombo cha kibilojia katika anga za juu
Iran imefanikiwa kutuma kapsuli ya kibilojia katika anga za juu kwa kutumia roketi iliyoundwa nchini na iliyopewa jina la Salman.
Kapsuli hiyo yenye uzito wa kilo 500, iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti wa Anga ya Iran, yenye uhusiano na Wizara ya Sayansi, Utafiti na Teknolojia, ilirushwa katika anga za mbali Jumatano katika eneo leny umbali wa kilomita 130 kutoka kwenye uso wa sayari ya dunia.
Kurushwa kapsuli hiyo ya kibilojia katika anga za mbali ni hatua ya kuwapeleka wanadamu katika anga za juu huku serikali ya Iran ikiwa na mpango maalumu wa kufufua sekta mbalimbali za tasnia ya anga za juu.
Tukio hilo la leo ni jaribio kwa teknolojia za anga katika sekta kama vile kurusha marekoti ya kubeba satalaiti, muundo wa aerodynamic wa kapsuli, na mifumo inayohusiana na udhibiti na ufuatiliaji wa hali ya kibayolojia.
Roketi la Salman limeundwa kikamilkifu katika Kiwanda cha Anga za Mbali cha Iran ambacho ni kampuni tanzu ya Wizara ya Ulinzi ya Iran na ambayo ina uwezo wa kuzindua bio-capsules yenye uzito wa kilo 500.
Licha ya vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi katika miaka ya hivi karibuni, Iran imeweza kupiga hatua kubwa katika mpango wake wa anga za juu za kiraia.
Kapsuli yake ya kwanza ya kibiolojia ya Iran iliyokuwa na kiumbe hai ilirushwa katika anga za mbali mwezi Februari 2010, kwa kutumia roketi ijulikanayo kama Kavoshgar.
Akizungumza na shirika la habari la Fars, waziri wa mawasiliano wa Iran Issa Zarepour alisema hivi karibuni Tehran itafanya majaribio ya kizazi kipya cha kapsuli za kibiolojia, ili kukaribia malengo yake ya ustawi wa sekta ya anga za mbali.
Iran ni miongoni mwa nchi 10 zinazoongoza katika tasnia ya anga za juu na kati ya 7 zinazoongoza katika anga za juu za anga.