Iran yakosoa Kongresi ya Marekani kuzuia uuzwaji ndege za Boeing
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i10831-iran_yakosoa_kongresi_ya_marekani_kuzuia_uuzwaji_ndege_za_boeing
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Marekani inapaswa kuondoa matatizo yanayoibuka nchini humo kuhusu utekelezwaji mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango wa Pamoja wa Utekelezwaji JCPOA.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 08, 2016 08:45 UTC
  • Iran yakosoa Kongresi ya Marekani kuzuia uuzwaji ndege za Boeing

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Marekani inapaswa kuondoa matatizo yanayoibuka nchini humo kuhusu utekelezwaji mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango wa Pamoja wa Utekelezwaji JCPOA.

Katika tamko rasmi baada ya Bunge la Kongresi nchini Marekani kupitsha sheria siku ya Alhamisi kuzuia Iran kuuziwa ndege za shirika la Kimarekani la Boeing, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Qasemi amesema: "Kwa mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kuna umuhimu mkubwa kwa upande wa pili kutekeleza ahadi zake." Amesema Iran haitilii maanani malumbano yaliyo ndani ya Marekani na kwamba serikali ya Marekani inawajibika kutekeeza ahadi zake katika mapatano ya nyuklia.

Qasemi amesema malumbano ya kimrengo Marekani katika kipindi hiki cha kukaribia uchaguzi wa rais ni jambo linalofahamika lakini ametahadharisha kuwa yamkini hitilafu hizo zikapelekea Washington kuvunja ahadi zake.

Makubaliano ya nyuklia ambayo yanafahamika kwa kifupi kama JCPOA na ambayo yalifikiwa Julai 14 mwaka uliopita kati ya Iran na madola sita makubwa duniani katika kundi la 5+1 yalitazamiwa kufungua ukurasa mpya katika uhusiano wa kisiasa na kiuchumi kati ya Tehran na nchi za Magharibi.

Hata hivyo, kama ilivyotarajiwa, Marekani imekuwa ikiweka vizingiti na kukiuka ahadi ilizotoa katika utekelezwaji wa mapatano hayo,