Kukua uchumi wa Iran licha ya kuandamwa na vikwazo
(last modified 2024-02-28T02:49:06+00:00 )
Feb 28, 2024 02:49 UTC
  • Kukua uchumi wa Iran licha ya kuandamwa na vikwazo

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limetangaza kuwa, uchumi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umekuwa kwa kiwango ambacho haikutabiriwa

Katika ripoti yake ya karibuni kuhusu hali ya uchumi wa dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limetangaza kuwa, ukuaji wa uchumi wa Iran mwaka 2023 ulikuwa wa asilimia 5.4. Ukuaji huo wa kutia moyo ulikuwa haujawahi kushuhudiwa tena katika miaka ya hivi karibuni, na ndio ukuaji mzuri zaidi tangu Marekani ilipojiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA mwaka 2018 na kuanza kutekeleza siasa za mashinikizo ya juu zaidi ya kisiasa na kiuchumi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ukuaji huo wa uchumi wa Iran wa asilimia 5.4 unaripiotiwa katika hali ambayo, kiwango cha wastani cha ukuaji wa uchumi duniani katika mwaka uliopita (2023) kilikuwa asilimia 2.6. Hii ni katika hali ambayo, chumi zilizoendelea duniani ukuaji wake wa kiuchumi mwaka jana ulikuwa asilimia 1.5 pekee. Kabla ya hapo, IMF ilikuwa imetabirii kwamba, ukuaji wa uchumi wa Iran katika mwaka uliopita ungekuwa wa asilimia 3.

Kwa mujibu wa Shirika la Fedha la Kimataifa, Iran ilikuwa na ukuaji wa juu zaidi wa uchumi mwaka 2023 kati ya nchi 30 za juu za uchumi duniani baada ya India. Nchi hizo 30, ambazo kwa pamoja zinachangia asilimia 83 ya uchumi wa dunia, zinajumuisha nchi zilizoendelea kiviwanda kama vile Marekani na Ujerumani na nchi zinazoendelea kama vile Iran, Uturuki, Korea Kusini na China.

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF)

 

Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limesema kuwa, sababu ya kukua kwa uchumi wa Iran katika mwaka uliopita ni kuongezeka kwa uzalishaji wa mafuta na kutangaza kuwa, uzalishaji wa mafuta wa Iran katika mwaka uliopita ulivuka mapipa milioni 2.7 kwa siku na hii inaashiria ongezeko la uzalishaji wa mafuta  wa mapipa 700,000 ikilinganishwa na hapo kabla. Mfuko wa Fedha wa Kimataifa pia umetangaza utabiri wake wa ukuaji wa uchumi wa Iran mnamo mwaka huu wa 2024 kwa kiwango cha 3.7%.

IMF imekiri kuongezeka kwa ukuaji wa uchumi wa Iran katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, huku sekta ya mafuta ikiwa ndio kichocheo cha maendeleo ya uchumi wa nchi, baada ya kuingia madarakani serikali ya awamu ya 13 ya Sayyid Ebrahim Raisi ambayo imeweza kuongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa mafuta licha ya vikwazo vya nchi za Magharibi na kuyashinda masoko mapya ya nje sambamba na kufidia nakisi ya bajeti na hivyo kuandaa uwanja wa ustawi wa uchumi na viwanda hapa nchini.

Hatua hizi zinachukuliwa huku majimui ya Wizara ya Mafuta na Shirika la Taifa la Mafuta la Iran hapo awali ziliweza kuuza takriban mapipa milioni 90 ya mafuta yaliyohifadhiwa na serikali iliyopita kupitia mazungumzo magumu, na rasilimali za fedha za kigeni zilizotokana na mauzo ya mafuta na gesi kuingizwa katika mzunguko wa uchumi wa nchi. Mtazamo wa utendaji wa mwaka mmoja wa sekta ya mafuta ya Iran unaonyesha ukweli huu kwamba, Shirika la Taifa la Mafuta la Iran limeweza kutekeleza vyema majukumu yake kwa kufanya maamuzi madhubuti na ya kistratijia na kupiga hatua kubwa katika ustawi wa Iran.

 

Kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotangazwa na Benki Kuu ya Iran ni kuwa, hisa ya mafuta na gesi katika ukuaji wa uchumi wa Iran ilikuwa takribani 20% katika kipindi hiki, ambayo ni hatua kubwa kati ya taasisi za utendaji na makampuni ya Iran.

Ukweli wa mambo ni kuwa, maamuzi ya serikali ya awamu ya 13 ya Jamhuri ya Kiislamu ya kubadilisha vipaumbele na malengo ya kiuchumi yamekuwa na matokeo chanya na ya kuridhisha katika kutatua changamoto muhimu za kiuchumi nchini.

Tags