May 02, 2024 11:21 UTC
  • Iran na Uganda zaazimia kupanua ushirikiano katika uga wa mawasiliano na teknolojia ya habari

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Iran ametangaza utayari wa taifa hili wa kushirikiana na Uganda katika miradi ya mawasiliano na teknolojia habari na uhamishaji wa taaluma hiyo kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.

Issa Zarepour amesema hayo hapa mjini Tehran katika mazungumzo yake na Rukia Isanga Nakadama, Naibu Waziri Mkuu wa Uganda aliyeko safarini mjini Tehran.

Waziri Zarepour ameashiria juhudi za Iran za kutafuta diplomasia ya kiuchumi katika bara la Afrika na juhudi za kupanua uhusiano wa kiuchumi na nchi za Afrika na kusema: Iran inajitahidi kuendeleza diplomasia ya kiuchumi katika bara la Afrika.

Amesema, makampuni ya ufundi na uhandisi ya Iran yametekeleza mipango muhimu ya miundombinu katika nchi mbalimbali za Afrika na zisizo za Afrika na iko tayari kutekeleza miradi kama hiyo katika nyanja za mawasiliano na habari nchin Uganda.

Ezatollah Akbari Talar Poshti, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Viwanda na Madini ya Bunge la Iran (kulia) akiwa katika mazungumzo na  Rukia Isanga Nakadama, Naibu Waziri Mkuu wa Uganda 

Kwa upande wake, Bi Rukia Isanga Nakadama, Naibu Waziri Mkuu wa Uganda  ameeleza kufurahishwa kwake na safari yake hapa mjini Tehran na kujionea kwa karibu uwezo wa Iran katika nyuga mbalimbali, na kutangaza utayarifu wake wa kutumia uwezo huo sambamba na maendeleo ya mawasiliano ya Uganda.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikitilia mkazo katika sera zake za kigeni juu ya kuimariisha uhusiano na mataifa ya Kiafrika, uhusiano ambao una msingi wa kuheshimiana na kuzingatia maslahi ya pande mbili.

Tags