May 05, 2024 04:17 UTC
  • Abdollahian: Utawala wa Kizayuni wa Israel kamwe hauwezi kuwa halali kwa kupita zama

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Utawala wa Israel si serikali halali na utawala huo wa kibaguzi unaoukalia kwa mabavu Palestina kamwe hauwezi kuwa halali kwa kupita zama.

Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema hayo katika hotuba yake kwenye mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).

Abdollahian amesisitiza kuwa, amani endelevu na ya haki itapatikana tu katika eneo hili tu kupitia kukomesha kukaliwa kwa mabavu Palestina, Syria na Lebanon, kurejea kwa wakimbizi wa Kipalestina katika nchi yao, na haki ya Wapalestina kuamua hatima yao.

 

Kadhalika Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa: Vuguvugu la wanaounga mkono Palestina duniani linazidi kuimarika kila siku baada ya miezi 7 ya vita vya utawala wa Israel dhidi ya Gaza, na limesambaa katika vyuo vikuu vya Marekani na kushuhudiwa harakati ya wanachuo kote Marekani ambako watu wanaojiita watetezi wa haki za binadamu duniani wanakandamiza sauti ya mwamko ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani. Vilevile amesema kuwa, juhudi za kieneo za kusitisha vita na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza hivi sasa zimeshika kasi.

Tags