May 07, 2024 02:19 UTC
  • Iran ni ya nne duniani kwa uzalishaji wa elimu katika uwanja wa mimea ya dawa

Katibu wa Kamati ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ya Mimea ya Dawa na Tiba Asilia katika Ofisi ya Rais wa Iran ametangaza kuwa, watafiti wa Iran wanashika nafasi ya nne duniani katika uzalishaji wa sayansi katika uga wa uzalishaji wa mimea ya dawa na tiba asilia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Mehr, Mohammad Reza Shams Ardakani, Katibu wa Kamati ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ya Mimea ya Dawa na Tiba Asilia katika Ofisi ya Rais wa Iran aamesema kuwa, kwa upande wa sayansi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi nzuri ya kisayansi na kivitendo na ya kukubalika kimataifa katika uwanja wa uzalishaji mimea ya dawa na tiba za kisunna.

Shams Ardakani sambamba na kueleza kuwa, historia ya matumizi ya mimea ya dawa na tiba asilia katika uwanja huo ni ya maelfu ya miaka, ameongeza kuwa, baada ya kuanzishwa shule za tiba asilia za Iran mwaka 2007, kulichukuliwa hatua za kasi katika nyanja ya uzalishaji wa sayansi na tangu miaka miwili iliyopita (2022) Iran imekuwa katika nafasi ya nne duniani hadi sasa.

 

Aidha amesema, mafundisho mengi ya tiba asilia ya Kiirani yamejengeka juu ya mtindo wa maisha na kutokana na ukweli kwamba, mafundisho hayo yamekita mizizi katika utamaduni wa watu yanaweza kukubalika vyema na huduma zake pia ni rahisi kwa watu kuzipata.

Katika miaka ya hivi karibuni na licha ya Iran kuandamwa na vikwazo vya kila upande na madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani, lakini imeweza kupiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kijeshi, kiulinzi, kitiba na kadhalika ikitegemea wataalamu wake wazawa.

Tags