May 10, 2024 10:09 UTC
  • Rais wa Iran: Makombora na uwezo wa kijeshi wa Iran haviwezi kujadiliwa

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa wajukuu wa Mtume wetu Muhammad (saw), Bibi Fatima Masoumah na kaka yake, Imam Ridha (as) na kusema: Kama ilivyosisitizwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, uwezo wa kijeshi na vielelezo vya mamlaka ya mfumo wa Kiislamu hapa nchini haviwezi kujadiliwa au kufanyiwa biashara kwa njia yoyote ile.

Sayyid Ebrahim Raisi aliyasema hayo jioni ya jana katika mjumuiko mkubwa wa wananchi wa mji mtakatifu wa Qum ulioko umbali wa zaidi ya kilomita 150 kusini mwa jiji la Tehran. 

Raisi ameeleza kuwa, mara kwa mara, maadui wa Jamhuri ya Kiislamu wamejaribu kukwamisha maendeleo ya taifa la Iran kwa kuanzisha ghasia, mashambulizi ya kigaidi, milipuko na njia nyinginezo na kuongeza kuwa, taifa la Iran limezima njama hizo zote kwa irada ya chuma na kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu SW. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaja operesheni ya kuuadhibu utawala wa Kizayuni wa Israel iliyopewa jina la Ahadi ya Kweli kuwa ni dhihirisho la nguvu ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu na kusema kuwa, masuala ya nchi yanaendelea vyema kwa kutegemea mantiki ya kimapinduzi na kupinga diplomasia ya kuombaomba.

Sehemu ya makombora ya Iran

Sayyid Ebrahim Raisi amepongeza mapambano ya miezi saba wa watu wa Ukanda wa Gaza dhidi ya adui Mzayuni mwenye sifa za mbwa mwitu na kusisitiza kuwa, licha ya jinai zisizo na idadi zinazofanyika katika Ukanda wa Gaza, lakini wananchi wa eneo hilo wanaendelea kupata ushindi katika uwanja wa vita kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, na hatimaye dui Mzayuni atashindwa.

Tags