May 22, 2024 07:09 UTC

Waislamu nchini Tanzania wameshiriki katika hafla ya kuwakumbuka na kuwaenzi viongozii wa Iran walioaga dunia hivi karibuni akiwemo Rais Ebrahim Raisi.

Waislamu wa Tanzania wamefanya kumbukumbu ya maombolezo ya kumuenzi Rais wa Iran aliyeaga dunia Ebrahim Rais pamoja na maafisa wengine aliokuwa ameambatana nao akiwemo waziri wake wa mashauri ya kigeni Hussein Amir-Abdollahian.

Maombolezo hayo yaliyoambatana na khitma ya Qur;an kwa ajili ya mashahidi hao yamefanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dar es Salaam.

Washiriki wa kumbukumbu hiyo mjini Dar es Salaam wamemtaja shahidi Ebrahim Rais kwamba, hakuwa Rais wa Iran tu bali alikuwa mwakiilishi wa watu wote wanaodhulumiwa duniani.

Image Caption

Wazungumzaji katika hafla hiyo wamemtaja Ebrahim Raisi kama mwanasiasa aliyekuwa na misimamo thabiti ambaye hakusita kutetea haki na alikuwa mstari wa mbele kutetea taifa madhulumu la Palestina.

Hafla hiyo iliyoongozwa na mwambata wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania Dr. Mohsen Maarefi ilihudhuriwa na shakhsia na viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislamu nchini humo.

Tags