May 26, 2024 07:11 UTC
  • Iran yapongeza maadhimisho ya

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amepongeza na kutoa mkono wa kheri kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Afrika (Africa Day).

Ali Bagheri Kani Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba, maadhimisho ya Siku ya Afrika yanakumbusha mshikamano, udugu na kuasisiwa Umoja wa Afrika urithi wa kudumu kwa ajili ya vizazi vijavyo.  

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema anataraji kuwa Umoja wa Afrika (AU) utapiga hatua na maendeleo na mataifa ya Afrika yatanufaika pakubwa kwa kuzingatia fursa na suhula nyingi za bara hilo. Tarehe 25 mwezi huu imepewa jina la Siku ya Afrika. 

Tarehe 25 mwezi Mei mwaka 1963 Umoja wa Nchi Huru za Afrika yaani Organization of African Unity (OAU) uliasisiwa; na katika siku hiyo wakuu wa nchi 30 kati ya nchi huru za Kiafrika 32 walisaini hati huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia kwa ajili ya kausisi umoja huo, na siku hii inaadhimishwa kila mwaka ili kudumisha umoja na mshikamano barani Afrika. 

Waasisi wa OAU 

 

Tags