Jul 31, 2024 03:53 UTC
  • Ismail Haniyeh ameuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi mjini Tehran

Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetangaza kuwa mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) Ismail Haniyeh na mmoja wa walinzi wake wameuawa shahidi baada ya kushambuliwa makazi yao mjini Tehran.

Taarifa ya Idara ya Uhusiano wa Umma ya IRGC imesema: Ismail Haniyeh, mkuu wa Idara ya Siasa ya Hamas, na mmoja wa walinzi wake wameuawa shahidi wakati makazi yao yalipopigwa mjini Tehran.

Sababu na undani wa tukio hili vinachunguzwa na matokeo yake yatatangazwa baadaye.

Wakati huo huo harakati ya Hamas pia imesema katika taarifa yake kwamba Ismail Haniyeh "ameuawa kutokana na hujuma ya kihaini ya Wazayuni dhidi ya makazi yake mjini Tehran."

Ismail Haniyeh alikuwa mjini Tehran jana (Jumanne) kushiriki katika sherehe za kuapishwa Rais wa Serikali ya Awamu ya 14 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tags