Aug 16, 2024 11:51 UTC
  • Aboutorabi Fard: Wazayuni lazima tutawatia adabu

Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa, kutiwa adabu utawala wa Kizayuni ni jambo lisiloepukika na watu wote wanaelewa vyema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitoziacha jinai hizo zipite hivi hivi.

Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Mohammad-Hassan Aboutorabi Fard amesema hayo leo katika khutba za Sala ya Ijumaa hapa Tehran na kusisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni na Marekani zinashirikiana katika jinai za Ghaza kama zilivyoshirikiana kwenye mauaji ya Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS na kwamba, majibu ya Iran kwa jinai hizo ni jambo lisiloepukika, lakini ni Tehran ndiyo itakayoainisha wakati wa kutiwa adabu Wazayuni.

Imam huyo wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa, hivi sasa pia Wazayuni wamefeli mbele ya mikakati na stratijia makini za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS aliuawa shahidi pamoja na mlinzi wake moja tarehe 31 Julai mwaka huu katika shambulio la kigaidi lililofanywa na Wazayuni mjini Tehran.

Mara baada ya jinai hiyo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisisitiza kuwa, Tehran italipiza kisasi damu za mgeni wake huyo azizi na haitoacha vivi hivi kuvunjiwa heshima haki yake ya kujitawala.

Tags