Sep 17, 2024 03:05 UTC
  • Rais Pezeshkian: Hakuna mjadala kuhusu ulazima wa kukabiliana na Israel

Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana alifanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aliposhika hatamu za uongozi akimrithi Sayyid Ibrahim Raisi aliyaeaga dunia katika ajali ya helikopta mwezi Meio mwaka huu.

Katika mkutano uliohudhuriwa na waandishi na maripota 300 wa ndani nan je, Daktari Pezeshkiana amezungumziia masuala mbalimbalii ya ndani na nje.

Rais Pezeshkian amesema, hakuna mjadala kuhusui ulazima wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel ili usiruhusiwe kukiuka sheria za kimataifa na za kibinadamu.

Kuhusu uhusiano na Saudi Arabia, Rais wa Iran amesema: Nitajaribu kuimarisha mafungamano ya udugu baina ya majirani zetu kwa mujibu wa maagizo ya Mtukufu Mtume (saww), na tutajaribu kuimarisha mafungamano na uhusiano na utawala wa Saudi Arabia pia.

 

Kuhusu sera ya Rais wa Jamhuri ya kuimarisha uhusiano na nchi jirani, ikiwa ni pamoja na Uturuki, Masoud Pezeshkina amesema: Uturuki ni nchi yenye urafiki na udugu kwetu, na tuna uhusiano mkubwa na uhusiano unaofanana na Uturuki inaweza kufikia Pakistan na Afghanistan kupitia Iran. Tunaitegemea sana Uturuki na nchi zingine za Kiislamu.

Aidha ametaka kufutwa kwa mipaka baina ya nchi jirani na kusema kuwa jambo hilo linatokana na wito wa Uislamu wa kuwa na umoja baina ya Waislamu, na lengo la wito wa kufutwa mipaka kati ya nchi jirani ni kuziendeleza nchi za eneo na kutatua matatizo ya nchi zao. Kadhalika amepuuza madai dhidi ya Iran ya kutuma makombora huko Yemen.