Zarif: Njama za Israel na Saudia za kuichafua Iran zimefeli
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i12031-zarif_njama_za_israel_na_saudia_za_kuichafua_iran_zimefeli
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudi Arabia zinaendeleza mradi wa propaganda chafu za kuidhihirisha Iran kuwa ni tishio.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 26, 2016 12:24 UTC
  • Zarif: Njama za Israel na Saudia za kuichafua Iran zimefeli

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudi Arabia zinaendeleza mradi wa propaganda chafu za kuidhihirisha Iran kuwa ni tishio.

Dakta Muhammad Javad Zarif ambaye yuko katika safari ya kuzitembelea nchi kadhaa za magharibi mwa Afrika amewaambia Wairani waishio nchini Ghana kwamba njama za kueneza hofu kuhusu Iran zimegonga mwamba japokuwa bado zinaendelea kwa kutumia ghara kubwa za Wazayuni na wanaoitakia mabaya Jamhuri ya Kiislamu hususan utawala wa kifalme wa Saudia.

Dakta Zarif amesema, njama hizo za kutaka kuchafua sura ya Iran zinafanyika kwa shabaha ya kuficha siasa mbovu za pande hizo huko Syria na Yemen. Ameongeza kuwa, baada ya miaka 37 sasa dunia imetambua kuwa, hatari halisi inayoukabili ulimwengu ni uwahabi na mitazamo ya kitakfiri. 

Daesh na washirika wake

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema jinai na ukatili mkubwa unaofanyika Yemen na Syria umewatumbukiza walimwengu katika huzuni kubwa. Ameongeza kuwa, ushirikiano wa tawala mbili zinazofanana za Israel na Saudi Arabia umefichuka kwa walimwengu na hauwezi kufichika tena.

Katika upande mwingine Dakta Zarif amesema, safari yake katika nchi kadhaa za Afrika inaonesha mwelekeo wa Jamhuri ya Kiislamu wa kutaka kupanua zaidi uhusiano wake na nchi za bara hilo.