Kutoka makundi yenye uhusiano na NATO hadi makundi ya muqawama Palestina
Parstoday- Mhadhiri wa Chuo Kikuu wa Iran na mwanaharakati wa mtandao wa kijamii wa X ameandika ujumbe katika ukurasa wake na kueleza mgawanyiko wa makundi yenye uhusiano na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) na makundi ya muuqawama.
Sayyid Mohammad Marandi, profesa na mkurugenzi wa Idara ya Lugha ya Kiingereza na Fasihi katika Kitivo cha Utafiti wa Masuala ya Ulimwengu cha Chuo Kikuu cha Tehran, ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X: Al-Qaeda, Daesh, Jolani na Baghdadi wameletwa na NATO, ambao kimsingi wanafadhiliwa zaidi na madikteta wa kifamilia na utajiri mkubwa wa mafuta na gesi.
Kulingana na mtandao wa Parstoday, Marandi aliandika katika muendelezo wa ujumbe wake huu: Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas), Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina, na harakati nyingine nyingi za muqawama ni za Kisunni na zimejitolea pakubwa kwa ajili ya watu wa Palestina.