Rais wa Iran kufanya safari nchini Tajikistan
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121026-rais_wa_iran_kufanya_safari_nchini_tajikistan
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni anatarajiwa kufanya safari ya kikazi nchini Tajikistan.
(last modified 2025-01-05T00:07:06+00:00 )
Jan 05, 2025 00:07 UTC
  • Rais wa Iran kufanya safari nchini Tajikistan

Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni anatarajiwa kufanya safari ya kikazi nchini Tajikistan.

Spika wa Bunge la Tajikistan ametangaza kuhusu ziara ya hivi karibuni ya Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dushanbe.

Rustam Emomali, Spika wa Bunge la Tajikistan na Meya wa Dushanbe, alitangaza jana (Jumamosi) kwa kuchapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kwamba Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian hivi karibuni anatarajiwa kufanya safari ya kikazi nchini Tajikistan.

Spika wa Bunge la Tajikistan ameongeza kuwa, safari hii itajumuisha mikutano kati ya marais wa nchi hizo mbili na mazungumzo mengine muhimu kati ya pande hizo mbili.

Chanzo cha habari katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Tajikistan pia kililiambia shirika la habari la Russia Novosti kwamba rais wa Iran atafanya safari nchini Tajikistan mwezi huu wa Januari.

Hii itakuwa safari ya kwanza ya Rais Pezeshkian nchini Tajikistan tangu alipochukua hatamu za uongozi Julai 28 mwaka jana alipoibuka na ushindi katika uchaguzi wa mapema kufuatia kifo cha Rais Ibrahim Raisi

Rais wa Tajikistan pia alifanya safari ya kikazi Tehran mnamo Januari 30, 2024, na Iran na Tajikistan zilitekeleza makubaliano ya kufuta visa kwa wamiliki wa pasi za kawaida mnamo Agosti 10 ya mwaka jana.