Iran: Tutatumia njia zote kuuwajibisha utawala wa Kizayuni kwa kuushambulia ubalozi wetu
(last modified Wed, 02 Apr 2025 11:59:22 GMT )
Apr 02, 2025 11:59 UTC
  • Iran: Tutatumia njia zote kuuwajibisha utawala wa Kizayuni kwa kuushambulia ubalozi wetu

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya jinai iliyofanywa na utawala wa Kizayuni ya kuushambulia ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu mjini Damascus na kutangaza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeazimia kutumia fursa na njia zote kutekeleza uadilifu na kuuwajibisha utawala wa kigaidi wa Israel.

Mnamo siku ya Jumatatu, Aprili 1, 2024, utawala wa Kizayuni ulifanya shambulio la makombora kutokea eneo la Miinuko ya Golan unayoikalia kwa mabavu na kulenga jengo la ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus na kuwaua shahidi Jenerali Mohammad Reza Zahedi, Jenerali Mohammad Hadi Haj Rahimi na wenzao watano.
 
Kwa mnasaba huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa ya kuenzi kumbukumbu ya Mashahidi wa shambulio hilo la kigaidi dhidi ya ubalozi wa Iran mjini Damascus na kusisitiza kwamba, kupita kwa muda hakutaweza katu kusahaulisha jinai hiyo na vitendo vingine vya kijinai vya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya taifa la Iran na mataifa ya eneo hili.
 
Taarifa hiyo imesema: shambulio la kijeshi na kigaidi la utawala wa Kizayuni dhidi ya ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus lilikuwa ukiukaji wa wazi wa kanuni za Hati ya Umoja wa Mataifa hususan kanuni inayopiga marufuku utumiaji mabavu; na ni ukiukaji mkubwa pia wa kanuni na taratibu za sheria za kimataifa hususan Mkataba wa 1961 wa Mahusiano ya Kidiplomasia na Mkataba wa 1973 unaohusu kuzuia na kutoa adhabu kwa makosa yanayofanywa dhidi ya shakhsia wanaolindwa kimataifa.
 
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeeleza bayana kwamba, kuendelea kukaa tu bila kuchukua hatua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya ukiukaji wa sheria usio na idadi na unaoendelea kufanywa kila leo na utawala wa ubaguzi wa apathaidi wa Kizayuni ndio sababu kuu inayoupa jeuri na uthubutu utawala huo ya kuendeleza ukiukaji wa kupindukia wa sheria na kanuni za kimataifa, haki za binadamu na sheria za masuala ya kibinadamu.../